Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Yaani kuanzia zoezi la Uchaguzi limeanza nimekuwa nikiwahoji wafanyakazi kijanja janja kujua kama watampigia kura nani - kuanzia Urais hadi udiwani. Kwa wafanyakazi kama 35 ambao nimewahoji kata ya Idukilo kwa kweli wanagugumia moyoni na kichini chini tu. Wote kwa URais kwa kweli wamekichoka chama chetu. Hawa wanasema kwa chini chini sana kuwa wamechoka na hawatapigia CCM kura. Clips za Tundu Lissu kwenye whatsapp groups kwa kweli zinawapa faraja sana. Kama alivyoongelea kuwapandishia mishahara wafanyakazi kwa kweli wanapata faraja sana.
Wafanyakazi wanajua fika kuwa vyama vyao vya wafanyakazi vimewekwa mifukoni. Havifurukuti. Wanajua fika kuwa wanatumbuliwa, wananyanyaswa, hawalipwi kwa wakati, kuna upendeleo lukuki n.k. Kuna tabaka limejiweka kama mungu watu - wanalipiza kwa wale walioonekana waliishi eti kama malaika - sasa waishi kama mashetani. Wafanyakazi hawasafiri nje ya nchi, hawana tena ubavu wa kujenga hata mabanda tu. Mikopo lukuki, mwenyewe nawadai zaidi ya milioni 60. Wanaonekana wote mafisadi tu
Walimu ndiyo walikuwa waathirika wakubwa wa vyeti feki. Hawa wamefundisha hadi baadhi ya mawaziri. Kuna wale Kulwa na Doto Biteko wamefundishwa na mwalimu mmoja yupo kati ya kijiji kimojawapo hapa kwetu - eti kaondoshwa na cheti feki. Yaani Cheti feki kato Waziri halafu anaondoshwa kwa aibu bila hata fedha alizochangia za pensheni kulipwa. Kuna wengine wawili waliondoshwa na kukutwa na stroke na tayari wametangulia mbele za haki.
Wapo madakatari na hata manesi waliochoma sindano baadhi ya mawaziri wakapona walipokuwa wanaumwa hoi vitandani lakini wameondoshwa kwa aibu. Ubaya wale ambao walihusika kuwaajiri hawa hawajachukuliwa hatua zozote. Zoezi hilo lilifanywa kwa upendeleo mkubwa - kina Bashite na baadhi ya watu au kada wameendelea kuachwa.
Tumesahau katika kila jamii kuna watu wakosaji na wema ili ukamilifu wa kibinadamu uwepo - kama walifanya makosa hawakupaswa kuadhibiwa vikali hivyo. Hatupo kamilifu. Hawa wote hata kama wana kura moja moja uongozi huu usitegemee kura zao. Kwa kweli wananchi walioathiriwa amiasha yao kutokana na ndugu zao kuwa wafanyakazi walionyanyasika kwa namna yeyote ile CCM hatuna ujanja na kura zao hatuzipati. Watu wameumia sana sana. Wapo kimya wanasubiri Tar. 28 Oktoba kwa hamu. Na wakitumika kusimamia Uchaguzi wengi watatugeuka CCM. Wanasema kimoyomoyo.
Tundu Lissu hata afikiriwe kama hana athari na Chama changu - ukweli watu wanasali Mungu amsimamie na Mwenyezi Mungu ni wa ajabu Tundu Lissu anaweza akawa Rais. Wapiga kura wa mwaka huu hawapo tofauti na wajumbe wa CCM. Its too late kuwarudisha waipende CCM tena. Hata uwapandishie dau la mshahara leo. Wameshaamua. Subirini tuone.
Tila Lila - Idukilo- Kishapu - Shinyanga.