Nawafikishieni Ujumbe Mnaoendesha IST na Vitz

Bodaboda wanakera sana. Mtu unawakwepa kulia na kushoto safari nzima!
Achana na sisi... tupo kama visisimizi tunapita popote. Na ukitubana sidemirror halali yetu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao unaozungumzia wewe, yaani wenye Vitz,IST halafu nyumbani mmeacha Prado,Fortuner sio walengwa wa Mh alietoa hii kauli.
 
Dah hiyo engine anaitesa mno! Yani anaichosha vibaya sana kwa upumbavu tu.

Daaah kabisa hawa jamaa wamekariri vibaya,sijajua mantiki ya kuwacha gari masaa mawili au matatu inaunguruma kama wafanyavyo madereva wa gari za serikali ,kama wanahofia joto si kama robosaa wanataka kuondoka si wanawaisha ili icool?
 
Acha hasira, ungemwelewa kwanZa Bwana Lema
 
Wanavaa tishirt za jezi au formsix wakishapiga na kaptura zile za draftidrafti au zile kaptura za pocket pembeni, kuta wanavaa visendoz na soksi na miwani juu, walipokaa vingereza vingi utahisi mipango ya kweli kumbe ni swaga tu hua nacheka sana
Wanaudhi sana mbwembwe kama zote
 
Sijawahi miliki gari ila kiukweli kabisa niliwahi jisemea moyoni sitanunua IST najichaga tu na kua mtulivu ila siku nikivuta chuma navuta chuma cha kiume haswa,pia napenda gari iliyopanda juu juu.
 
Tuna watu hawana akili lakini wako katika nafasi za uongozi. Sasa mwenzio kuendesha IST inakuuma nini? Mambo ya ajabu sana.
Nchi ngumu sana hii. Mtu mpaka unapangiwa gari ya kuendesha na matajiri wanaoendesha ma biemu dabiliyu na ma rolisi roisi. Sijui nikauze tu ka IST kangu nirudi kwenye mwendokasi? Si kwa dharau hizi dadeki!
 
nilikutana na mjuba mmoja na ist yake road ya tunduru-songea akaanza ligi.... hakuchukua hata saa moja namkuta kafungua bonet moshi kama anarina asali....
 
nilikutana na mjuba mmoja na ist yake road ya tunduru-songea akaanza ligi.... hakuchukua hata saa moja namkuta kafungua bonet moshi kama anarina asali....
Hahaaa. Eti kama anarina asali
 
Juzi kuna bodaboda nimegusa, we alitoa maneno, kigari chenyewe cha mkopo, IST nayo gari? Gari gani hii, mimi hata bure sichukui" nikashuka nikamtazama bodaboda mwenyewe anaedharua IST nikaishia kucheka tu.
Masikin huwa na maneno mabaya sana na makali,yanayoumiza mtima.
 

Nisamehe mkuuu kumbe ni wewe
 
Hii gari naikubali sana...sema wanaoendesha wana vurugu balaa! Ngoja leo nione wangapi wamevaa kaptura fupi
Kuna siku waliniboa Sana natoka zangu Moroco mbele yangu wako wa 2 wanatamba barabara mzima, kutembea hawatembei na site hawataki kunipa.

Nikajisemea kimoyo moyo hawa hawanijui, nikawaacha wakatangulia kidogo mora kama 50, nikashusha gia kwenye li Hardbody langu turubo ikafunguka nikalilazimisha katikati baada ya kuwaoita nikamwekea wakulima bodi then nakamrudishia wa kushoto. [emoji23][emoji23][emoji23] Walinikuta kwenye mataa ya Namanga nilikuwa nawazoomo wanavyotukana
 
Sijalizishwa na maneno ya Lema hata kidogo.

Akumbuke kabisaaa kazi yake ni kutetea wasio na maji, hospitali n.k hawa wa magari hawamuhusu
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mtuache tupumue! Wengine ndo kwanzaaa insurance ya kwanza hata haijaisha muda
 
Hii ni kweli kabisa na wengi wao ndio wanaanza kumiliki isitoshe ni mikopo
 
nilikutana na mjuba mmoja na ist yake road ya tunduru-songea akaanza ligi.... hakuchukua hata saa moja namkuta kafungua bonet moshi kama anarina asali....

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kha!!
 

My ribs! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna mwanasiasa kasema mkishanunua IST na VItz na kuanza kuvaa kaptura fupi weekend mnajiona mmepatia sana maisha, mnajihisi ni middle class kumbe ni masikini wenye nafuu! Mjumbe hauwawi, weekend njema!
Dah kw maneno Ayo unaweza kujikuta mjumbe unauawa yan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…