MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Yanga ni timu inayo 'enjoy' sana kucheza katika space. Ni timu inayofurahia sana aina ya soka la 'kutembeza ball'. Ile falsafa ya coach Ramović ya 'Gusa achia twende kwao' haikuanza kwake, bali imekuwa falsafa ambayo naweza kusema ni ya Rais wa club, Eng.Hersi Said. Rais wa Yanga ni aina ya kiongozi anayehusudu soka la kutembea, ndiyo maana tangu alipochukua timu na kumpatia Nabi, aina ya wachezaji anaosajili, mpaka kwa huyu wa mwisho, Jonathan Ikangalombo ni aina ya wachezaji wenye kasi sana.
Sasa, tuje kwenye timu za ligi kuu pamoja na zile za club bingwa barani Afrika, ukitazama kwa umakini, Jambo ambalo timu nyingi za Ligi kuu, mfano Azam, Namungo, Mashujaa, Simba, KMC nk. Ukiangalia aina ya makosa wanayofanya yanayosababisha kufungwa ni yale yale na yanajirudia, kosa kubwa ni hili " KUTOMPATIA YANGA HESHIMA YAKE KAMA TIMU KUBWA" au kitaalam kukataa kuwa second team inapokutana na Yanga na kushindwa kucheza kwa mbinu na nidhamu.
Hakuna club Tanzania hata Afrika kiujumla yenye wachezaji bora kwa kuangalia ubora wa mchezaji 'mmoja mmoja' kama Yanga. Kama kuna timu zingine basi ni chache. Ndiyo maana ukichunguza timu zilizoifunga au kutoa sare ni timu zilizotumia mbinu zaidi na ziliingia kama underdog na kuiheshimu Yanga na si 'vuta nikuvute' wakitambua ubora wa wachezaji wa Yanga endapo wakienda bampa to bampa. Tazama mchezo dhidi ya Al hilal, MC Alger,JKT, Tabora utd,Azam (japo majeruhi yaliathiri mchezo) Ila wote hao waliingia kwa nidhamu na wakafanikiwa kuokota alama.
Ubora wa Yanga upo kwenye 'spaces' na wanaenjoy 'kutembeza ball' ukicheza na Yanga na wewe ukataka 'kutembeza ball' ni sawa na kupigana na mamba kwenye maji 😀 yeye ataenjoy zaidi, Refer michezo miwili dhidi ya Mamelodi sundowns, Kaizer chiefs au dhidi ya CR Belouizdad.Ndiyo maana wanasema Yanga ni hatari zaidi wasipokuwa na mpira, Unajua kwanini? Kwa sababu mara nyingi timu pinzani zinapomiliki mpira zinajisahau na kuachia 'spaces' na mara wanapopoteza mpira wanachelewa kuziba! Hapo ndipo uhatari ulipo!
Ukija kwenye Ligi kuu, tusidanganyane, Hakuna middle bora ya mpira kumzidi Aucho, Hakuna striker yenye nguvu na kasi kama Mzize, Hakuna ball dancer na box player kama Pacome zouzoa, Max Nzengeli, Hakuna beki zinazoshuka na kutoa killer pass kama Yao kouassi, na mwenye speed kama Chadrack Boka, hapo sijazungumzia booster zingine kama hiyo Ikangalombo.Hakuna namba 10 hatari na yenye msuli kama Aziz ki, Chama, achana na Mudathir. Hao wachezaji sio tu kwenye ligi bali ni wachezaji bora sana Afrika katika nafasi zao na wanaanza kikosi chochote cha kwanza Afrika.Siku wakiamka vizuri wakacheza katika 100% ni hatari tupu kwa timu isiyotaka kuwaheshimu.
Sasa kwa ubora huo wa mchezaji mmojammoja, baadhi ya timu hazishtuki na hazitaki kucheza kwa heshima na nidhamu, Zinataka kwenda kiulalo ulalo! Halooo 😀
Hakuna timu yenye uwezo wa kufunguka na kwenda kiulalo ulalo na Yanga! Ukifanya hivyo utaambulia 6,2,3,1,5 zinasoma kwenye ubao 😀