Rogie
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 7,586
- 6,697
Wadhamini wa Ligi Kuu Ya Tanzania Bara, kampuni ya mitandao ya simu ya Vodacom, imekabidhi mfano wa hundi ya Tsh 1,000,000/= kwa mshambuliaji wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi siku ya leo Septemba 19.
Okwi amekabidhiwa hundi hiyo baada ya kutangazwa kuwa mchezaji wa bora wa ligi hiyo ijulikanayo kama Vodacom Premier League kwa mwezi Agosti akiwa amepachika mabao manne kwenye mwezi huo wa Agosti, akifunga mabao hayo yote kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.
Zoezi hilo la kukabidhi limefanyika kwenye ofisi za Vodacom ambapo Okwi alikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Meneja Chapa wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma na Afisa Udhamini, Ibrahim Kaude.
Mara baada ya kukabidhiwa mfano huo wa hundi Okwi hakusita kuficha mahaba yake kwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, pamoja na kiungo Thaban Kamusoko ikiwa ni swali aliloulizwa juu ya mchezaji gani anamkubali zaidi kwenye ligi.
“Kwa Tanzania klabu nyingi zina wachezaji wazuri lakini nje ya Simba kuna mchezaji anaitwa Kamusoko ananivutia sana na Donald Ngoma pia,” alisema Okwi.
Okwi ametwaa tuzo hiyo ya uchezaji bora mwezi Agosti baada ya kuwabwaga wapinzani wake, Boniface Maganga kutoka Mbao FC na kiungo Mohamed Issa kutoka Mtibwa Sugar.