Nawakumbuka na siwezi kuwasahau

So sad...pole sana, we all do that n sometimes it isn't easy to explain
 
kwa kwel bro umenihuzunisha sana kwa simulizi yako,na wewe ukanifanya ni flashback 2003 oct...nilipompoteza mdogo wng mpendwa,namkumbuka sana,nilimpenda sana,he was respecting me much as his bro,but unfortunately akatutoka...natembea na picha yake(passport) ktk wallet yng,kila nnapofungua kutoa hela naona sura yake nzuri.R.I.P young bro...always in my mind.
 
Pole sana.
Umenikumbusha my late bro, 20 years now and still feels like yesteryear. Tulikuwa tunapendana sana. I felt safe with him, nikihisi anaweza kupindua dunia kwa ajili yangu.
Siku moja alikuwa anaumwa sikio, hakwenda shule. Nikiwa std 2, naenda shule saa tano. Wakati namuaga nikaona analia, nikakaa pembeni yake na begi yangu ya madaftari na kuanza kulia nae. Mara maza akaingia, akatuuliza mnalia nini? Nikamuambia kaka anaumwa sana. Alinikimbiza kama mwizi! Its a sweet memory of pure love!
Ofcoz mom is 8 years gone, I miss them all together.
 

R.I.P kibol young bro, Pole sana.....Tupo wengi tuliowapoteza tunaowapenda and sad thing hatuwezi kuwarudisha. Kikubwa ni kuwaombea God knows
 
Last edited by a moderator:

Pole sana na wewe & R.I.P King'asti bro and mother............So sweet and sad memories. Hata mimi nakumbuka my bro ambaye nimemsema alikuwa hawezi kula kama sipo atanitafuta kokote napocheza na kuniita, fun thing alikuwa anapenda sana dagaa, aiseee anaweza kupewa pesa na baba afuate nyama buchani akajifanya kusahau na kununua dagaa. Na ndiye aliyenifanya nikawapenda sana.

Nakumbuka pia alipokuwa anasoma sekondari akibaki na pocket money lazima aniletee madaftari na kalamu tena yale makubwa. Na nilijua tu braza akija lazima atakuja na chochote.

Siku mama alifariki alitamani kuruka ukuta wa nyumba......so sad
 
Last edited by a moderator:
Mwenyezi mungu awape Amal njema na usichoke kuwaombea hiyo ndio itakua sadaka Yao kwako, binfsi namkumbuka Sanaa Mama yangu alifariki miaka 9 ilopita,juu yakua ni mda mwingi lakini napata tabu
Sana kwani hakua mama tuu alikua ndio msiriwangu, rafiki, na sifanyi chochote bila kumshauri yeye,
Lakini namsukuru sanaa kwa malezi yake na daima ntakaa nimshukuru na kumuombea mungu lakini kwakweli
Sina msiriwangu tena zaidi ya Mwenyezi mungu.......
 
Mkuu, umefanya la maana sana kuweka topic hii. Si umeona watu tunavyofarijiana?? Yaani unajisikia kuwa kumbe masahibu hayako kwako tu. Bravo!!
 
Siosiri umeniliza, baba yangu nilimpenda na nitamkumbuka daima,ni miaka 23 toka afariki lkn haipiti siku bila kumkumbuka, mimi nilikua kipenzi chake kati ya wanawe, nakumbuka kabla hajafariki aliagiza wanawe twende kumwona babu yangu akakataa akidai hadi tufunge shule,siku moja NIKAMVIZIA BABU SIKU ANASAFIRI NIKAMFATA NYUMANYUMA HADI STENDI ALIPOINGIA KWENYE GARI NAMI NIKAINGIA NIKAJIFICHA[nilikua chekechea],tukasafiri wote hadi kijijini NILIPOFIKA BABA ALIFURAH SANA AKAITA MPIGAPICHA TUKAPIGA PICHA masaa 8 baadae alifariki dunia.
 

Kweli ulikuwa unampenda, nafikiri Babu alijilaumu kwa nini hakukubali mwanzo. R.I.P Angel Msoffe Father
 
Last edited by a moderator:
Sitaki hata kukumbuka maana, mhh......

Pole WALIMWEUSI lakini si vibaya mara mojmoja kuwakumbuka tuliowapenda......kuna vitu tunajifunza. Just imagine kwa mfano unamfanyia mtu kitu kibaya lakini unaporudisha kumbukumbu nyuma unamkumbuka baba/mama/dada au kaka alivyokuwa hapendi tabia hiyo.......bila shaka utajifunza.

Lakini hii pia ni njia nzuri ya kuwafariji wengine........Kuna watu wanafikiri wana mikosi kuliko wote Duniani kumbe wakisikia ya wenzao wanashusha pumzi.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu huwa nikikumbuka siwezi zia kulia, its almost 15 years since MY BELOVED ONE AND ONLY Brothe passed away, mbaya zaidi he die in my arms o, mh, RIP brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…