Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwa kwel bro umenihuzunisha sana kwa simulizi yako,na wewe ukanifanya ni flashback 2003 oct...nilipompoteza mdogo wng mpendwa,namkumbuka sana,nilimpenda sana,he was respecting me much as his bro,but unfortunately akatutoka...natembea na picha yake(passport) ktk wallet yng,kila nnapofungua kutoa hela naona sura yake nzuri.R.I.P young bro...always in my mind.
Pole sana.
Umenikumbusha my late bro, 20 years now and still feels like yesteryear. Tulikuwa tunapendana sana. I felt safe with him, nikihisi anaweza kupindua dunia kwa ajili yangu.
Siku moja alikuwa anaumwa sikio, hakwenda shule. Nikiwa std 2, naenda shule saa tano. Wakati namuaga nikaona analia, nikakaa pembeni yake na begi yangu ya madaftari na kuanza kulia nae. Mara maza akaingia, akatuuliza mnalia nini? Nikamuambia kaka anaumwa sana. Alinikimbiza kama mwizi! Its a sweet memory of pure love!
Ofcoz mom is 8 years gone, I miss them all together.
Nilipata ndoto juzi usiku iliyohusisha familia yetu, Leo asubuhi nikawa natafakari nayoyakumbuka wakati walipokuwa hai na pia kushare na wanajamvi nayoyakumbuka:
Baba
Ni marehemu takribani miaka 16 imepita. Mkimya na mkarimu…….mchapakazi hasa, alikuwa anakula "ngano" lakini ni wachache mno wangejua kama ni mtumiaji. Nakumbuka utotoni alishawahi kunichapa mara moja tu…..nilipokataa kunyoa nywele.
Mama
Mama yangu alifariki takribani miaka 13 iliyopita. Asubuhi ya leo nikawa nakumbuka jinsi alivyotulea familia ya watoto watatu na nyakati zingine extended family inaongeza idadi na hata kufikia saba au nane.
Maisha yalikuwa ya kupanda na kushuka lakini angalau hatukuwahi kulala njaa. Nakumbuka enzi hizo Baba alipokuwa hana kazi jinsi mama alivyokuwa anapiga hesabu zake ndani….mboga kiduchu, unga haba lakini tunamshukuru Mungu tunamanga nguna bila kumbagua yeyote ndani na kila mtu anaridhika.
Mpole na anyependa sana watoto wake, lakini si kwamba fimbo hatukuzipata la hasha panapo makosa hasa mimi nakumbuka alikuwa ananichapa on the spot ingawa sikuwa mtukutu viile.
Kaka yangu
Naye marehemu. Katika simulizi za mama mara kwa mara tukiwa wadogo alikuwa akisema wakati huyu kaka yangu akiwa mdogo kama umri wa miaka 3 alikuwa akimsumbua na kumuuliza kila wakati kwa nini yeye hana mdogo wake wakati wenzie wanacheza na wadogo zao?
Baada ya kuzaliwa mimi pengine kuliko watoto wote nilipata mapokezi ya kifalme kutoka kwa kaka yangu………..naambiwa ikiwa nitalia kdogo tu nitabembelezwa na kupewa nachotaka. Alinibeba, kuniosha na kunipikia, Kusema ukweli kaka yangu alinilea vizuri sana (wakati mwingine wazazi wangu walikuwa wanenda kutafuta rizki na kuniacha).
Sijui wewe unawakumbuka kwa lipi watu waliokupenda
Siosiri umeniliza, baba yangu nilimpenda na nitamkumbuka daima,ni miaka 23 toka afariki lkn haipiti siku bila kumkumbuka, mimi nilikua kipenzi chake kati ya wanawe, nakumbuka kabla hajafariki aliagiza wanawe twende kumwona babu yangu akakataa akidai hadi tufunge shule,NIKAMVIZIA BABU SIKU ANASAFIRI NIKAMFATA NYUMANYUMA HADI STENDI ALIPOINGIA KWENYE GARI NAMI NIKAINGIA NIKAJIFICHA,tukasafiri wote hadi kijijini NILIPOFIKA BABA ALIFURAH SANA AKAITA MPIGAPICHA TUKAPIGA PICHA masaa 8 baadae alifariki dunia.
Sitaki hata kukumbuka maana, mhh......
huwezi jua nimekumiss kias gani father,r.i.p my beloved dadKweli ulikuwa unampenda, nafikiri Babu alijilaumu kwa nini hakukubali mwanzo. R.I.P Angel Msoffe Father
Pole WALIMWEUSI lakini si vibaya mara mojmoja kuwakumbuka tuliowapenda......kuna vitu tunajifunza. Just imagine kwa mfano unamfanyia mtu kitu kibaya lakini unaporudisha kumbukumbu nyuma unamkumbuka baba/mama/dada au kaka alivyokuwa hapendi tabia hiyo.......bila shaka utajifunza.
Lakini hii pia ni njia nzuri ya kuwafariji wengine........Kuna watu wanafikiri wana mikosi kuliko wote Duniani kumbe wakisikia ya wenzao wanashusha pumzi.