Hamjambo!
Kuna sisi nilikuwa nataka kuwapa watu fulani hivi. Ila nimezuiwa na wahenga. Nimeambiwa mara nyingi natoa codes fulani ingawaje vichwa panzi wamekuwa wagumu kuzipata frequencies zangu ili kung'amua codes hizo.
Leo sina maneno mengi.
Nitawarejelea wahenga wakisema DUA LA KUKU DAIMA DAWAMU HALIMPATI MWEWE.
Msiwe Wajinga.
Maisha ni kuchagua. Kutawala au kutawaliwa.
Kulaumu au kulaumiwa.
Predators au preys
Sikiliza. Nisikilizeni.
Niliambiwa na wazee wangu kamwe nisipende kujipa matumaini ya uongo. Kwani hiyo itanipa gonjwa baya la kushindwa kufanya maamuzi sahihi magumu.
Wazee waliniambia kuwa Dua la kuu halimpati mwewe kwa sababu siku zote Mwewe yupo Mbinguni na Kuku yupo ardhini.
Kuku ni Kuku tuu.
Kuku ni chakula cha Mwewe tuu.
Kuku hata ategemee msaada wa binadamu kamwe dua lake halitampata Mwewe.
Kwa sababu Kuku sio tuu chakula cha Mwewe. Bali pia ni chakula cha binadamu anayemfuga. Sasa iweje Dua la kuku limpate mwewe?
Binadamu na Mwewe wote ni walaji wa Kuku. Kuku hilo halijui. Kuku atashtaki kwa Binadamu kuwa Mwewe anamla anasahau binadamu naye siku ya maulid na Christmas atamchinja na kumla. Looh! Salaleee
Sasa nikakumbuka Habari za Dua la albadiri. Nikakumbuka kuvunja jungu.
Nikamkumbuka Wajina wangu Robert Amsterdam, nikakumbuka ICC, nikasahau Bunge la Ulaya,
Dua la Kuku ni Dua la Kuku tuu. Mwewe, kipanga, Tai na Tai wala mizogo(vultures) wao hawapatwi na hayo maombi ya kuku.
Siku moja nikamuuliza Mhenga mmoja hivi. Hata Kuku wafunge na kuomba dua lao halitasikiwa?
Nikajibiwa Dua la Kuku halitajibiwa hata siku moja hata watoe Kafara la damu.
Kwa nini?
Kwa sababu Kuku huishia kuomba tuu.
Kuku humuachia mungu wake(binadamu) wakati naye anasubiria siku able.
Kwa sababu kuku anaakili lakini anapoteza kumbukumbu. Maskini
Kuku. Akili anayo lakini anasahau papohapo baada ya tukio likiisha.
Sababu nyingine iliyoniliza.
Iliyonimaliza. Iliyonifanye nimuonee huruma Kuku.
Ati kuku akiliwa kifaranga chake na mwewe moyoni mwake husema atataga mayai mengine kisha ataangua vifaranga vingine.
Na atasubiri dua lake litimie. Hatimaye anashangaa siku moja isiyo na jina akikimbizwa na binadamu anayemfuga.
Kisha analazwa shingo pembeni miguu ikiwa imebanwa. Kuku Ancona kisu, kuku analia sio kwa sababu anachinjwa nope! Bali ni kwa sababu alishindwa kujua Binadamu na Mwewe ni adui zake na wote wanamuona kama chakula.
Tofauti ni kuwa Binadamu ni adui anayemhudumia na kumlisha. Adui wa karibu mwenye ukarimu na upole.
Mwewe ni adui wa mbali asiyemkarimu wala upole.
Poleni sana Kuku.
Mhenga aliniambia, waambie wale wenye kutaka kuambiwa. Kwenye maisha yao wasije chagua kuwa Kuku. Wawe Mwewe. Ikiwashinda wawe Kenge, ikiwashinda wawe kicheche. Kama haitoshi wawe Tai.
Niacheni nipumzike.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam