Nawakumbusha tuliwahi kumsajili beki mmoja akiitwa Mohamed Ouattara lakini tukaishia kumtukana, tusubiri uwanjani ndio tuwasifie

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Ukimuona Mohamed Outara unaweza sema timu imepata beki wa maana sana, Simba iliwahi kumsajili beki huyo kutoka sudan.

Tulimsifia mnooooo, tukasema tumepata beki.

Siku ile alipozungushwa na Fiston Mayele tukapigwa na utopolo ndipo thamani yetu kwake ilipoishia.

Outtara alikuwa na mwili jumba, lakini alikuwa mzito balaa.

Kutokana na hilo simba ikamweka benchi hadi alipoletwa Inonga Bacca kushika nafasi yake.

Leo tumeletewa beki anaitwa Chamou Karaboue kutoka Ivory Coast.

Ni beki mrefu sana, ana nguvu na ni mbabe.

Ila uchezaji wake ni kama yule beki wa Yanga mzanzibar anayeitwa Ninja.Chamou ni zaidi ya Ninja, yeye kumdondosha mtu ndani ya penalt box ni kawaida tu.

Tuombe mungu
 
Mwache awadondoshe tutadaka hizo penati. Zimbwe alizungukwa na Guede akabaki amesimama, hakuna aliyesema kitu achilia mbali lile shuti "alilompasia" kipa wake Ayoub tena mechi hiyo hiyo.

Outtara anamzidi mara 100 Kennedy na hana tofauti sana kiuchezaji na Mwamnyeto.
 
Kwa Mpira wa Kariakoo...usajili na uhlisia wa baadaye uwanjani...na Hatma ya mnyaziMungu...Mnakumbuka Kambale,no Kambole!
 
Ukimuona Mohamed Outara unaweza sema timu imepata beki wa maana sana, Simba iliwahi kumsajili beki huyo kutoka sudan.

Tulimsifia mnooooo, tukasema tumepata beki.

Siku ile alipozungushwa na Fiston Mayele tukapigwa na utopolo ndipo thamani yetu kwake ilipoishia.

Outtara alikuwa na mwili jumba, lakini alikuwa mzito balaa.

Kutokana na hilo simba ikamweka benchi hadi alipoletwa Inonga Bacca kushika nafasi yake.

Leo tumeletewa beki anaitwa Chamou Karaboue kutoka Ivory Coast.

Ni beki mrefu sana, ana nguvu na ni mbabe.

Ila uchezaji wake ni kama yule beki wa Yanga mzanzibar anayeitwa Ninja.Chamou ni zaidi ya Ninja, yeye kumdondosha mtu ndani ya penalt box ni kawaida tu.

Tuombe mungu
Umeashauriwa sana umfuate jamaa yako Chama alikoenda kuliko kuendelea na ramli zako chonganishi dhidi ya Simba..
Utakuja kupata aibu.
 
Back
Top Bottom