Nawaomba radhi Watanzania kwa kushiriki kumuweka Madarakani Malinzi

Nawaomba radhi Watanzania kwa kushiriki kumuweka Madarakani Malinzi

Mwacheni Malinzi amalizie ngwe nyingine. Hii mipango ya kipindi kimoja kimoja inakuwaga sio endelevu. Mwache andeleze programs za soka alizozipanga.
 
Nilikuwa mmoja wa wadau wa soka tuliopambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba Jamal Malinzi anashinda urais wa TFF , Tulipambana kwa udi na uvumba , Kwa hali na mali hadi tukafanikiwa .

Lakini kwa madudu yaliyotokea kwenye uongozi wake , nimeona nijitokeze mbele yenu ndugu zangu kuwaombeni sana radhi kwa hujuma hii tuliolifanyia soka la Tanzania , mtoto akinyea mkono usiukate , Naahidi sitorudia tena kufanya madudu ya kumbeba mtu yeyote asiye na uwezo kwa vile tu ni Mfanyabiashara mwenzangu .

Wito wangu kwa wadau wa soka wa Tanzania , hakikisheni mnachagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza , na mwenye kuzijua hasa changamoto za soka la nchi hii.

Niko tayari kusaidia upande wowote wa kambi ya mgombea yeyote mwenye weledi na mwenye maono ya kusukuma soka la Tanzania mbele zaidi.

Mungu ibariki TFF .
Malinzi yuko selo Oysterbay polis anashikiliwa na Takukuru kwa matumizi mabaya ya ofisi....
 
Tumerudi nyuma hatua mia kwenye maendeleo ya soka letu tutakukumbuka daima Chila Tenga
 
Malinzi yuko selo Oysterbay polis anashikiliwa na Takukuru kwa matumizi mabaya ya ofisi....
Nakushukuru kwa Taarifa mkuu , niko njiani kwenda kumtoa , kabla ya jioni atakuwa huru .
 
Wewe kaa pembeni na tunashukuru sana kwa msaada wako kipindi kile,kwa sasa tupo wengine tuliojitolea kumuweka tena ili amalizie yale mazuri aliyoyaanzisha japokuwa wewe huyaoni.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
nilikuambia kuhusu faili lake Mr Malinzi pale Upnga ukabisha, sasa ataungana na wengine kujibu tuhuma
 
Nasubiria thread ya kujuta kumpigia kura Lowasa..na kuendelea kuisupport Chadema.
 
Watu wanaojiita wa mpira wengi ni wapigaji tu,kwa hali ilivyo ss namshauri wallace karia ajitoe kwenye uchaguzi,maana nae ni mpigaji aliyetokea kwenye tundu ya sindano kwenda kunyea ndoo na boss wake malinzi
 
Back
Top Bottom