Binti yangu amemaliza Elimu ya sekondari na kufaulu kwa Pointi 12 katika masomo yote. Katika kutafuta Shule nzuri ya kuendelea na Elimu yake ya kidato cha tano yeye akanishauri kuwa anataka kwenda Canossa kuwa ni shule nzuri ingawaje mimi sina taarifa kamili kuhusu Shule hii. Amefanya mtihani na tayari amechaguliwa japo na shule zingine kama Maria Goreti pia amechaguliwa. Ninawaombeni wana Jamii forums kunipa ushauri ni wapi nimshauri aende?