Ndugu zangu wadau wana Jf na watanzania wenzangu
Kwa kinachoendelea Dodoma kama busara haikutumika, tutegemee wajumbe wa bunge la katiba wakifungasha virago na kuodoka zao bila kukamilisha kilicho wapeleka dodoma. Hii inatokana na vifungu namba 37 na 38 kutokufikiwa mwafaka mpaka sasa, watanzania tulitaraji kazi hiyo ingehitimu leo, lakini pamoja na mwenyekiti wa muda kuunda kamati maalumu ya maridhiano na mwafaka, bado mpaka sasa hakuna kilichofikiwa na badala yake wale walioona bunge la leo jioni tumeshuhudia mwenyekiti akivivuka vifungu hivyo nilivyovitaja cha 37 na 38 kuwa kamati ya maridhiano na mwafaka bado haijamaliza kazi yake.
Ndugu kimbuka vifungu hivi ndo vile vinavyo amua upigaji kura ya WAZI au ya SIRI.Hapa ndo naona watanzania wenzetu wajumbe wa bunge maalumu la katiba wanashindwa kuafikiana na baadhi kuanza kuondoka zao makwao. Kama mtanzania mwenye mapenzai mema na taifa letu kwa imani zaetu tuombe kwa ajiri ya taifa letu kama kuna watu wenye nia ovu washindwe.
UPDATES
Wadau awali nilidhani nijambo la kawaida lakini sasa kwa kinachoendelea Dodoma kuna kila sababu zinazotaia shaka kuwa huenda ni ya ccm si njema katika zoezi zima la mchakato wa katiba mpya.
Ndugu zangu tukumbuke kuwa utamaduni wetu wa upigaji kura kitambo sasa umekuwa ni wasiri, jambo linalo mpa uhuru mutu kuammua atakakacho, si mbali ni majuzi tu tumeshuhudia mwenyekiti wa muda bwana Kificho akipatikana katika mchakato wa upigaji kura uliohusisha kura ya siri. Kwanini zinajengeka hisia kuwa nia ya ccm ni OVU? Ni kwa sababu utamaduni wetu wa upigaji kura umekuwa ni wa siri, sasa wenzetu wanatuondoa kwenye utamaduni tulio uzoea na kutuambia kuwa huo ndo msimamo wao.
Kama mtakumbuka mwenyekiti wa muda aliunda kamati maalum kwa ajiri ya mwafaka na maridhiano na mashauriano, katika kamati hiyo inamuhusisha waziri mkuu Mh Pinda, mwenyekiti wa CUF Lipumba na mwenyekiti wa CDM Mbowe, katika hali isiyo ya kawaida ukweli ni kwamba wenzetu hawa wa kamati ya maridhiano walishindwa kufikia maridiano kwa kilichoitwa msimamo wa CCM. Pia mtakumbuka kuwa juzi Bunge liliahirishwa mpaka jana mchana saa9 Alasiri ili kutoa muda kwa kamati ya maridhiano kufikia mwafaka, kwa vifungu vilivyo achwa wazi makusudi bila kupitishwa, vikiwemo vile vyenye ukakasi ambavyo ni kifungu cha 37 na 38 vinavyo amua upigaji kura SIRI au WAZI.
Tunaambiwa kuwa kikao cha wabunge wa CCM kilicho kaa juzi saa 2 usiku na kukamilisha mazungumuzo saa 5:30 kilikuwa na lengo la wajumbe wa kamati ya maridhiano kutoa mrejesho juu ya kilicho fikiwa kuhusu uamuzi wa upigaji kura ya SIRI au WAZI, mwnyekiti wa kikao hicho alikuwa ni waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya kufungua kikao alimkaribisha mjumbe wa Halimashauri kuu Mh Vuai Nahodha ili kutoa mrejesho wa maendeleo ya kamati ya mashauriano. Jambo alilo waambia wajumbe wa kikao hicho cha CCM kuwa kwa jinsi mazingira yalivyo nje na ndani suala la upigaji kura wa SIRI hauepukiki, na hapo ndo alisimama Ole Sedeka na kusema hawataki kisikia kura ya SIRI vinginevyo nikuiondoa CCM kwenye msimamo wa serikali 2. Seandeka alimwambia waziri mkuu kuwa kama atathubutu kuridhia upigaji kura wa SIRI awe tayari kuwajibishwa na chama. Na hapa ndo waziri mkuu wanatajwa kufunga kile kiao cha wabubge wa CCM kwa kusema kuwa kuanzia sasa msimamao wa chama ni kura ya WAZI na sivinginevyo.
Ndugu zangu hapa mtaona kwamba msimamo wa CCM ndo unatia shaka watu ndani na nje ya bunge la la katiba sasa wanaanza kuona ni wazi kuwa nia ya CCM katika hili si njema hata kidogo. katika misimamo huo wa CCM na makundi mengine wakiwemo wapinzani sitarajii mwafaka endapo kila kundi litasimama kideta kwa kile kinachoitwa msimamo usiyoyumbishwa. Nahapa ndo baadhi ya makundi yataamua kususa na kuondoka Dodoma. Ukivuta nikavuta hakika itakatika
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.