Christmas ya leo nimefanya reserve baadae tupate mtoko pamoja na familia lakini bado sina furaha,
- Mwaka mzima huu sijarudi kwetu, Kijijini kwetu huwa tunarudi wote kwa pamoja kukiwa na msiba tu
- watoto wangu nimewahi kuwapeleka mara mbili tu huko kwao, mara ya mwisho ilikua 2020, kwa lugha nyepesi ni kwamba hawajapazoea kwao na nahisi washasahaulika na wao wamepasahau,
- Huku mijini ndugu tunakutana wenye nafuu ya maendeleo mtu ana nyumba yake na kausafiri lakini kule kijijini maendeleo yaliyofanyika ni kubadili bati tu.
- Kijijini kiujumla hali za wanajikijiji ni mbaya, Ni matajiri wawili tu wamejenga nyumba zinazoeleweka lakini kuna nyumba za nyasi nyingi, barabara mbovu, maji ya bomba hakuna, n.k.
Tukija kwa wachaga nawaonea wivu maana hawasahau kwao, kila mwaka wanarudi kwao "KWA PAMOJA" yani wale waliotawanyika mikoani na nje ya nchi wanarudi kwao, na hii inasaidia hata watoto wapazoee kwao na wao kuendeleza utamaduni, si tu hivyo bali huchochea maendeleo, kuikuta nyumba ya nyasi uchagani ni sawa na kutafuta punje ya mchele kwenye tope.