Nawapenda watoto kuliko mume

Nawapenda watoto kuliko mume

Ni mvivu anapenda kulala, kuangalia TV, na hata kama nina shughuli watoto wakaomba msaada kwake, atawaambia kamwambieni au msubirini mama. Nitajitahidi kumshirikisha. Asante sana Klorokwini.

Mi sioni kama kuna tatizo, specially mzee mwenyewe kama ni mtu wa kujivuta vuta. Watoto wengi wanasaidiwa sana kama mama anakuwa strong kwahiyo wasaidie watoto wenu wawe responsible, ili siku moja mzee ajichukulie sifa zote kwamba bila yeye nothing would happen. Angalizo: Yale mambo mengine usimsahau ni ya muhimu sana.
 
I have heard you. My case is I love kids more than hubby. I want to learn how to overcome this situation.

Lewinski pole sana jamani, didn't know ! In anycase I think you diverted all attn to kids coz he wronged you
And he has to regain that trust

Jaribu kuwa na activities ambazo yabidi mfanye kama couple pia kucheza na watoto ni muhimu,

Pole sana na ninakuombea yote haya ni majaribu ya ndoa
 
mi naona ulishajua tatizo lako na unajua pia namna ya kulikabili. hakuna njia ya mkato utakayoweza kuipata hapa JF, bali check your psychological factors. ushauri wa kloquine wa kwanza kabisa ni mzuri sana kuzingatia. mi naongeza kuwa kupenda watoto ni vizuri sana na kuwajibika kama mama mwingi wa mapenzi nyumbani ni vyema sana tena inapendeza na unastahili pongezi na keep it up. ila naona umeyafanya maisha ya nyumbani kwako kuwa sawa na nusu family ingawa una familia kamili. siku utakapoondokewa na huyo mume wako (siombei) ndio utagundua umuhimu na uzuri wake. please my dear learn to live as a family.

kama unaweza tafuta msaidizi hapo nyumbani kwako ili nawe upate muda wa kupumzika. lakini sioni ubaya wa baba kukusaidia mfano kuandaa nguo zake (hata na zako) za kazini kama ratiba yako ya majukumu ndiyo hiyo na huna msaidizi wa kazi, ila inapokuja kuwa kila siku unajirusha kitandani mapema na kuanza kusinzia bila kutaka hata kubadilishana mawazo na mwenzako japo kidogo, mwenzio atahisi kukosa accompany yako. atakuwa mpweke na kama Mungu hataingilia kati anaweza hata kuanguka dhambini na kuleta balaa nyumbani mwako. so take care, otherwise tuambie kwa nini hisia zako ziko mbali na mtu uliyemridhia mwenyewe kuishi naye. kama baba ni uvivu (kama ulivyosema mahali fulani) ni vidosari vidogovidogo tu, vihandle with care, visije vikaitumbukiza nyumba yako katika magomvi mengi na yasyoisha na probably hata kuivunja siku moja. asiyezba ufa hujenga ukuta. wewe tayari umeuona ufa, so kazi unayo ya kuziba hizo nyufa mapema.

Sidhani kama kuna mwanamke anapenda kugawa familia. Hata hivyo ningekuwa nafurahia hii hali nisingekuja kuomba ushauri hapa. Tunakula pamoja, tunachit chat hapa na pale tukiwa nyumbani, tunatoka kwenda kutembelea ndugu na jamaa kama familia. Pia tunashare intimacy pale inapotakikana kufanya hivyo ingawa nahisi ufanisi wangu umepungua kiasi. Ila kinachonitatiza ni kwamba moyoni nahisi niko more involved and in love na watoto kuliko baba yao. Ushauri kama wa Klorokwini na wengine nimeupokea kwa mikono miwili na nitaufanyia kazi.

kumfumania nako yawezekana kulikuathi kisycolojia

Nilishamsamehe na najitahidi kusahau. Ni majaribu ya ndoa kama alivyosema Nsiande.
 
Nilimfumania live akifanya mapenzi na baba watoto, chumbani kwangu, kitandani kwangu. Nilimsamehe baba watoto na nilijiwekea msimamo kuwa sitaweka msaidizi nyumbani.

hapo ndipo palipoharibu psycholojia yako dada. ile picha haijawahinikuta but lazima itakuwa the worst in ones life. pole sana. ila kama ulikuwa umeishaanza kupay less attention hata kabla ya kumfumania, huenda lonelyness ilimpa majaribu ya kumbaka huyo HG. kama kila siku mnaye chumbani na wewe huna fellowship naye anaimiss hata accompany yako, hata maongezi yanakuwa ya mgao, kweli hapo kama hana displine ya Mungu, atatokea kuanza kumuona HG kama option nyingine

Well, why housegirl ni tatizo kuliko suluhisho?, well there are things which I as a mother can't avoid doing but there are things that simply have to be done by a HG !!
Kwamfano wote tunatoka saa kumi na moja tuanze foleni from Mbezi kuelekea makazini na nina mtoto wa miezi 10 nyumbani, huyu namwachia nani kama si HG ?
Pia hawa wakubwa wakirudi toka shule saa 9 nani atawapikia kama si HG ??
The only day my HG rests is sunday and I take charge of cooking and everything
Jaribu kumshirikisha baba watoto kwenye homework, pia shuleni kuna sports day and school open activities zinazoencourage watoto na wazazi, hizo tunaenda sote na mume wangu
Kama leo jpili, HG yuko off mtoto mdogo yuko na baba na wakubwa wananisaidia upishi

What I really think, u have certain insecurities in your life,am thinking the fact that you do everything yourself is potray 'the superwoman attitude' which depict 'the perfect wife ' you have also brushed off having a housegirl as it brings more problems which answers your insecurities in trustin someone else doing what you are doing
Unless ur work is not involving..but some of us have to travel with little ones and an extra help..

I could go on and on, but you may PM me for further talks on this
Mhandisi


nashukuru dada mhandisi, naona mwenzangu una uzoefu na mambo ya nyumbana umempa practical experience. ni ushauri mzuri, lewinsky na nakushauri umPM kwani hakika hapa utachota na hata kujaza kikapu. ubarikiwe sana mhandisi Nsiande. inaonekana nyumba yako ni nzuri na ina furaha ya Bwana
 
hizo activities zote unazofanya na watoto..
kwa nini usimjumlishe na mume..

kama ni homework wewe na yeye mnawasaidia watoto..
hapo mwa weza kumaliza mapema na kupata muda muaafaka pamoja..
au kama kupika wote muingi jikoni....
 
ukikaa naye chini ukamweleza haya uliyoandika hapa, hatakuelewa na kukubali kujishughulisha nao zaidi?
 
Cant See any problem with That You are a Mother...... Uchungu wa Mwana.......

KIDS ARE YOUR TRUE BLOOD MUME SIO NDUGU YAKO........ THESE ARE TWO DIFFERENT KINDS OF LOVE MOTHERLY LOVE NA HUSBAND LOVE TOTALLY DIFFERENT NA KAMA VINAFANANA THEN YOU NEED HELP........

Samahani kwa kushout i wanted to make my point clear
 
i know it can be tricky but try to find time for your husband too....otherwise akienda nyumba ndogo you will have yourself to blame........
i think km uko occupied sana na kazi za nyumbani,seek some sort of help! housegirl/housemaid can be the solution you need!.......
kubali sometimes na wewe ni normal human being you cant be super-hero-woman that you can do everything by yourself,admit you need some help na mambo yatakuwa smooth.
 
House girl tena?! I will never ever hire one kwani nina hakika hili ni tatizo zaidi kuliko suluhisho.

Je unaushauri mwingine zaidi?

Tafuta House girl ambaye ni mtu mzima kakuzidi umri awe miaka 48 au zaidi ambaye hata mvutia mumewe. Angalau aje mara tatu kwa wiki kukusaidia kazi na kuondoka asilale nyumbani kwako. Ili upate muda mahsusi na Mzee. Pia jaribu kupata ushauri kutoka kwa rafiki zake wa karibu au wakwe zako ili aongeze ushirikiano kwa watoto. Usijaribu kufanya kazi zote ambazo baba anatakiwa kuzifanya kwa watoto. Kila lakheri!
 
Tafuta House girl ambaye ni mtu mzima kakuzidi umri awe miaka 48 au zaidi ambaye hata mvutia mumewe. Angalau aje mara tatu kwa wiki kukusaidia kazi na kuondoka asilale nyumbani kwako. Ili upate muda mahsusi na Mzee. Pia jaribu kupata ushauri kutoka kwa rafiki zake wa karibu au wakwe zako ili aongeze ushirikiano kwa watoto. Usijaribu kufanya kazi zote ambazo baba anatakiwa kuzifanya kwa watoto. Kila lakheri!



Mh...!!! Huu ushauri nitamuomba muomba ushauri asiupokee,kwa umri ulioutaja hapo nina uhakika kabisa huyo HG atakuwa msimbe,na ni nani asiyejua tabia za wasimbe?
 
Mtafutie mumeo shughuli ya kufanya inaelekea yupo tu nyumbani anaangalia tv. Nafikiri hata hicho kitu kinakuboa ndio maana anapoteza mvuto.
Ni sawa na mwanaume awe anatoka nyumbani asubuhi akirudi jioni anakuta mkewe mchafu hajaoga, nyumba chafu na vitu havipo katika mpangilio lazima huyo mke apoteze mvuto kwa mumewe.
 
I have heard you. My case is I love kids more than hubby. I want to learn how to overcome this situation.
Forgive me maybe am dumb and I dont understand.... whats wrong in loving your kids more? also is motherly love same as love for the husband? and if you like to spend more time with kids than husband just tell him them maybe you, him and the kids can spend time together.

Maybe the issue is if you say you dont love your husband anymore.... children love should always be there, the heart can accomodate many peoples love, am sure you still love your parents, relatives and friends... though you love the differently. If I have not understood you please correct me.
 
I have heard you. My case is I love kids more than hubby. I want to learn how to overcome this situation.

Inabidi ubadilike ili hali hii isiendelee kuwepo au inaweza kuathiri ndoa yako. Kuhusu mwenzio kutopenda kushiriki katika activities nyingi za watoto ongea naye na kumwambia umuhimu wa yeye kushiriki mara nyingi kila hali inaporuhusu badala ya kuangalia TV, kulala kwa kifupi aache uvivu. Pia anaweza kukusaidia kwenda kufanya shopping za groceries ili kukupunguzia wewe kazi zako za kila siku. Mianaume mingine mhhhhhh! (samahani Lewinsky kwa kuandika hili)
 
Wakati mwingine mambo tunayokutana nayo katika maisha hasa ya mahusiano hupelekea hali hizi, tafuta muda japo siku moja muwe wawili tuu sehemu iliyotulia pasiwe na mtu mwingine yoyote then kila mtu ktk hali ya utulivu amshauri mwenzake wapi ameona hapajakaa sawa ili aparekebishe, mkiendelea kuwa hivyo utawaathiri watoto ambapo watabase upande wako na mwishoni hawatamthamini baba yao.
 
........Pole weee!! Kazi zote hizo peke yako,lazima upendo uwe hafifu kwa mumeo. Ila naweza kusema hiyo tabia umeifuga mwenyewe tokea day 1 ulipoanza kuishi naye. Ulitakiwa kumuelekeza kazi za kukusadia tokea enzi za uchumba wenu, hata baada ya kuolewa na kuzaa angeendelea tu kukusadia kazi.

Mie naona hapa umeelemewa na kazi kiasi kwamba hata muda wa kukaa pamoja kama mume na mke hakuna.........unachoka mno shost.Upendo kwa watoto ni muhimu tena sana na wewe kama mama ndio haswa wakujenga familia bora......ila usisahau upendo kwa mumeo kiasi hicho.

Anza kumtuma baadhi ya kazi kufanya huyo, tena mtume kwa kudeka kabisa kwamba honey nimechoka nisaidie kunyosha, au kufua.Mpe orodha chakula unachotaka ili aende kununua supermarket .........taratibu kama ni mwanamme muelewa ataanza kukusaidia kazi.

Siku hizi maisha tunayoishi ni modern family hivyo kazi ni kusaidiana........kama yeye ni mwajiriwa na wewe mwajiriwa pia hivyo mambo ya nyumbani kusaidiana.
 
House girl tena?! I will never ever hire one kwani nina hakika hili ni tatizo zaidi kuliko suluhisho.

Je unaushauri mwingine zaidi?

ur true woman.
gud.
hasu gal si suluhisho...weng wamelewa na kasumba i.
hongera kwa kuamka.
jtaid kumweka karibu...hamu itakuja tu..au havutiki ata km ukimshirikisha muwe pamoja wakat unacheza na watoto..?
 
Tafuta House girl ambaye ni mtu mzima kakuzidi umri awe miaka 48 au zaidi ambaye hata mvutia mumewe. Angalau aje mara tatu kwa wiki kukusaidia kazi na kuondoka asilale nyumbani kwako. Ili upate muda mahsusi na Mzee. Pia jaribu kupata ushauri kutoka kwa rafiki zake wa karibu au wakwe zako ili aongeze ushirikiano kwa watoto. Usijaribu kufanya kazi zote ambazo baba anatakiwa kuzifanya kwa watoto. Kila lakheri!


Au atafute ndugu wa mume ndio awe anasaidia kazi hapo nyumbani. Sidhani kama mume atamtokea ndugu yake.
 
Back
Top Bottom