Pre GE2025 Nawapongeza CHADEMA kwa kupiga vita rushwa ya CCM kama walivyopigana vita ya kilichoitwa kuunga juhudi mkono

Pre GE2025 Nawapongeza CHADEMA kwa kupiga vita rushwa ya CCM kama walivyopigana vita ya kilichoitwa kuunga juhudi mkono

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Chadema ni chama kinachosimamia maslahi ya umma bila kujali kupoteza viongozi. Kwa namna chadema inavyojipambanua ndivyo CCM inavyozidi kuonekana kama hawana nguvu ya kukemea rushwa.

Tundu Lisu na Mbowe kwa pamoja wameweka agenda mezani; wakapanga safari na kuanza kazi. Baada ya kuanza kazi na kwa uungwaji mkono wanaopata viongozi wa CCM wakasitisha mikutano na kurudi Dodoma na DAR

Lakini pia agenda za hawa viongozi vimewekwa kulingana na mazingira....uchaguzi wa kanda ya kusini unapandisha joto la kisiasa na kutishia kabisa nafasi ya CCM MBEYA na Iringa.

CCM kwa kuona hivyo wakaja na mbinu za kuweka maandikizi ili kumpa Tulia ahueni lakini Lisu kaona huo mchezo. Amesimama adharani akakemea.

Chakushangaza CCM wamekuwa wakali kusikia Tundu anapiga vita rushwa; kila mmoja kwa nafasi yake ameandika kumpinga Lisu kwa maeneno yake yakipinga vita rushwa. Hata akina Mdee waliounga mkono juhudi wamekurupuka wakidhani wataonewa huruma badala yake wamepigwa mawe hadi wamekaa kimya

Uimara wa chadema ni pamoja na kuwapiga vita adharani viongozi wa CCM na mikakati yao. Kama walivyofeli kwenye juhudi ndicho wanachovuna sasa.....

Tundu songa mbele endelea kuwapiga wazidi kuchanganyikiwa
 
JamiiForums442997317_236x211.jpeg
 
Back
Top Bottom