Nawapongeza serikali Kwa ukarabati wa meli Ya MV Victoria Hapa kazi tu

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Mnyonge mnyongeni lakini hakini yake mpeni.

Leo nimesafiri na hii meli kutoka Mwanza kuelekea Bukoba kusema la ukweli nimefurahia safari. Meli inavutia mno seat ziko vizuri, huduma ya chakula, upande wa bar Kuna vinywaji na burudani hadi nimeisahau kama Niko safarini.

Wahudumu wameli wako vizuri na ni wakarimu mno. Wako tofauti na wahudumu wengine wa taasisi za umma.

Heko Kwa uongozi wa meli hii Kwa ubunifu wa huduma. Penye kusifia tusifie, penye kukosoa tukosoe

PXL_20240621_003712264.jpg
PXL_20240621_003748368.jpg
Pia soma:
 
JPM hiyo kanda alijitahidi sana kuwawekea miundo mbinu, sasa inabidi wajiongeze sponsor hayupo tena, hilo ziwa linahitaji speed boats pia ili safari ya Mwanza Bukoba na visiwa vyake vyote iwe masaa mawili, watu binafsi fursa hiyo, acha hayo mameli makubwa yabebe mizigo au watalii wa ziwa
 
Hii meli ina uzuri wote usema la ukweli, vyoo safi na huduma bora
 
Nilipo Ona Safari Lager nikasema ishaingia kichwani hio, kesho utaleta uzi wahudumu wa Mv Victoria wazuri kuliko wahudumu wa Air Tanzania🤣🤣
 
Tatizo kuna kunguni balaa
Nafikiri ilikuwa na kunguni kabla haijafanyiwa ukarabati, kama ni kweli ni swala la menejiment ya meli na itabidi wawajibishwe big time, kunguni ni issue ndogo sana Department ya usafi inaweza kumaliza hilo, sielewi kama mmiliki wa meli au mwendeshaji unawezaje kuachia kunguni mpaka watu walalamike, mtu lazima awajibike hapo ndio watajifunza
 
JPM hiyo kanda alijitahidi sana kuwawekea miundo mbinu, sasa inabidi wajiongeze sponsor hayupo tena, hilo ziwa linahitaji speed boats pia ili safari ya Mwanza Bukoba na visiwa vyake vyote iwe masaa mawili, watu binafsi fursa hiyo, acha hayo mameli makubwa yabebe mizigo au watalii wa ziwa
Tafiti ziwani nyasa na Tanganyika .....
 
Nafikiri ilikuwa na kunguni kabla haijafanyiwa ukarabati, kama ni kweli ni swala la menejiment ya meli na itabidi wawajibishwe big time, kunguni ni issue ndogo sana ya usafi inaweza kumaliza hilo, sielewi kama mmiliki wa meli au mwendeshaji unawezaje kuachia kunguni mpaka watu walalamike, mtu lazima awajibike hapo ndio watajifunza
We unachekesha kweli meli baada ya matengenezo ilianza kufanya safari zake 2021 na ndo huo mwaka nilipanda miezi ya mwanzoni kabisa kunguni walikuwemo ndo ijekuwa mwaka huu
 
Weeeee usiniambie sasa kama meli hadi wamasai wanapanda unafikiri itakosa kunguni kweli
Mtu kasafiri juzi tu ananibishia, treni yenyewe muda si mrefu wadau watapandikiza mbegu, ndo ije kuwa meli watu wanalala humo tena wakikagua vizuri hata chawa wamo
 
Mnyonge mnyongeni lakini hakini yake mpeni.

Leo nimesafiri na hii meli kutoka Mwanza kuelekea Bukoba kusema la ukweli nimefurahia safari. Meli inavutia mno seat ziko vizuri, huduma ya chakula, upande wa bar Kuna vinywaji na burudani hadi nimeisahau kama Niko safarini.

Wahudumu wameli wako vizuri na ni wakarimu mno. Wako tofauti na wahudumu wengine wa taasisi za umma.

Heko Kwa uongozi wa meli hii Kwa ubunifu wa huduma. Penye kusifia tusifie, penye kukosoa tukosoe

Pia soma:
Nawaasa serikali iendelee kufanya periodic preventive maintanance pamoja na kufata masharti yote ya uzito wa juu wa meli, Hatutaki Historia nyingine inayosababishwa na wandamu!
 
Mtu kasafiri juzi tu ananibishia, treni yenyewe muda si mrefu wadau watapandikiza mbegu, ndo ije kuwa meli watu wanalala humo tena wakikagua vizuri hata chawa wamo
We umekomalia kunguni.
Hii meli ni nzuri na kunguni hawamo.
Hata kama wamo, hupaswi kubeza kazi hii nzuri, hili meli lilipaki miaka kadhaa ila Sasa lipo kama jipya kabisa na Lina kasi nzuri.
Na Sasa nimeona wanapanua bandari ya Kemondo,
Mambo ni mazuri.
Serikali ikiongeza meli 1 itakuwa poa zaidi
 
Back
Top Bottom