Nawashangaa wanaosema Makonda anafaa kuwa Makamu wa Rais

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
4,042
Reaction score
6,854
Baada ya DW na BBC kumtangaza kwamba Nchimbi amejiuzulu,naanza kuamini kwamba hizi habari ni kweli.
Lakini watu wanasema ati Makonda awe VP.
This is absurd.
The man is arrogant.
Halafu ni mhalifu wa Kimataifa. Hata State Department wanajua.
Lakini wakati Wammasai wanalalamika kuporwa makazi yao,yeye akaenda Dubai.
Toka alivyorudi kutoka Dubai tunamuona anatabasamu sana.
Halafu tulimuona kapiga picha amempakata mdada fulani.
Ni Bora Nchimbi aendelee kuwa Makamu wa Rais.
Samia alikuwa ana hakika CCM hawamtaki.
Mbona basi aling'ang'ania kuwa Rais baada ya Magufuli kufariki?
 
Makonda hana hasa za kuwa hata Waziri.
Vile tu watu wanabebana.
 
Baada ya DW na BBC kumtangaza kwamba Nchimbi amejiuzulu,naanza kuamini kwamba hizi habari ni kweli.
Habari za kweli ni zile tuu zitakazotolewa na Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kinyume cha hapo ni tetesi tuu na fake news!.
Lakini watu wanasema ati Makonda awe VP.
Yes mtu yeyote mwenye sifa za kuwa mbunge, anaweza kuwa VP au kuwa rais. https://www.jamiiforums.com/threads...asababu-ana-uthubutu-kuliko-hata-jpm.1197731/
This is absurd. The man is arrogant.
Kuwa arrogant au kutokuwa arrogant sio miongoni mwa sifa za urais!.
Halafu ni mhalifu wa Kimataifa. Hata State Department wanajua.
Mtu kuwa mhalifu wa kimataifa hakumpotezei sifa za urais!, Uhuru alikuwa mhalifu, Al Bashir alikuwa mhalifu, Charles Taylor alikuwa mhalifu, na hata kile kilichotokea October 29, ICC wakitia timu, kuna mtu atatangazwa mhalifu, hakumz
Lakini wakati Wammasai wanalalamika kuporwa makazi yao,yeye akaenda Dubai.
Kwani yeye ndiye mlinzi wa makazi ya Wamasai?
Toka alivyorudi kutoka Dubai tunamuona anatabasamu sana.
Ulitaka anune?
Halafu tulimuona kapiga picha amempakata mdada fulani.
Kuna kosa lolote kwa mtu yoyote kumpakata mdada yoyote?
Ni Bora Nchimbi aendelee kuwa Makamu wa Rais.
Nchimbi bado ni VP mpaka ikulu itoe taarifa.
Samia alikuwa ana hakika CCM hawamtaki.
CCM gani hawamtaki?, zile kura milioni 32 ni za kina nani?
Mbona basi aling'ang'ania kuwa Rais baada ya Magufuli kufariki?
Ni aling'ang'ania au ni kwa mujibu wa katiba?

Kaka Mkubwa, at 73, big up sana kuendelea kuandika, nitakuja kukuona Butiama soon!.
P
 
Mimi nipo Dar.
Yule Makonda ni mhalifu.
Kwa muda wa miezi sita sasa tumekuwa tunasikia Nchimbi atajiuzulu na kwamba Makonda atachikua nafasi yake.
Itakuwa indecent kama Makonda aliwa replacement.
Anyone else isipokuwa huyo aliyekuwa anatajwatajwa.
Itaonekana ilikuwa njama.
 
Wewe bado unatupigia propaganda za kura milioni 32 za wizi,kuwa serious kidogo
 
Mkuu, mbona umemkaba sana kooni kaka yangu.
 
Wewe bado unatupigia propaganda za kura milioni 32 za wizi,kuwa serious kidogo
Mkuu Matawi, Matawi ya juu , mimi zaidi ya kuwa member wa JF, pia ni mwandishi wa habari, hivyo hata kama tunaujua ukweli halisi, katika kuripoti habari zetu, tunazingatia sana chanzo mamlaka, authoritative source, mfano tunajua lile tukio la Machi 17, 2021, lilitokea rasmi lini, ila likatangazwa ni Mach 17, tuna stick na March 17.

Hivyo hata uchaguzi mkuu wetu, tunajua kilichofanyika, lakini maadam mamlaka kuu ya uchaguzi ni NEC, na imesema mtu kashinda kwa kura milioni 32, then tunakwenda na ushindi wa kura milioni 32, hii sio propaganda ni taarifa rasmi ya chanzo mamlaka!.

P.
 
Kuwa serious kaka, kama " ulijua tukio la Machi 17 uhalisia wake na si TANGAZO lisilo sahihi , pia unajua UKWELI wa kura 32 mils na sio tangazo lake lilisilo sahihi.
Kuna haja ya kuamini kuwa
1. Uandishi wako wa habari hauna creditibility, na hatuitaji kuuamini maana una ripoti kile watu wanapanga na si ukweli wake si ni sawa?
2. Tukisema kaka yetu tunayekupenda kwa maandiko yako ni mnafiki tutakukosea?
3. Unatuaminisha kuwa unaweza kununulika useme chochote?
 
Mkuu Omu, Omulasil , uandishi wa habari ni fani yenye misingi na kanuni, moja ya msingi mkuu ni kusema ukweli, kuripoti ukweli, kuandika ukweli na kutangaza ukweli, tell nothing but the truth, report truthful with objectivity, impartiality, fainess and balance, ila kabla ya kuusema huo unaufanyia objectivity test, ukiusema ukweli huo utasaidia?, ukipima ukaona hausaidii, hata kama ni kweli, unashauriwa usiseme, usiandike, usitangaze.

Na katika kutangaza, tunatakiwa kutumia chanzo mamlaka!, mfano wewe chanzo mamlaka cha kukuambia baba yako ni nani, ni mama yako, hata ikitokea, nikashikwa sikio na baba yako halisi, na nikikuangalia ni copyright, siwezi kukuambia ukweli huo kwasababu mimi sio chanzo mamlaka cha baba yako ni nani!, mama yako akikumbia baba yako ni fulani, huyo ndiye baba yako hata kama aliyeipachika ni mwingine!.

Hili somo nimeliendesha sana tuu humu.

P.​

 
Mkuu P
Kunachangamoto kubwa sana naiona kutoka kwenye uandishi wako MZURI inayo athiriwa pakubwa na ufuasi wako wa kuwa mwana CCM

Wewe ni mwandishi mzuri wa chambuzi za Kisiasa Tanzania, siasa ambazo ni CHAFU sana dhidi ya watawala kwa upinzani

Natambua kwamba nafsi yako kuna sehemu kubwa haikubaliani na udhalimu huu lakini kuna sehemu iliyobaki bado inabeba u CCM wako……….. na hapo ndipo unapotumia kipengele cha “objectivity test” kuwa bias kwa kuufucha na kuto usema ukweli kwasababu kwa muono wa serikali ya CCM ukweli huo ni mwiba kwao

Na mara nyingi sana utakuta UKWELI huo ambao unaonekana “hausaidii wala kubadilisha jamii” unakua upo wazi kwa kila mtu ila ni mwiba kwa Serikali ya CCM tu na wala sio wananchi kama taifa

Speaking of Chanzo cha habari,
Mkuu chanzo kikuu cha habari za Serikali imekua ni Msigwa na matamko ya viongozi……….. kweli kabisa unaweza ku relay na vyanzo hivyo linapokuja swala la serikali kuboronga?
Kwamba wewe akina Msigwa ndio mwisho wako wa kuaminika wa habari linapokuja swala la serikali kuboronga?

Msigwa yeye ndiye anatakiwa ku apply hichi kipengele cha objectively test kwa kuufucha ukweli kama msemaji lakini kazi yako kama mwandishi ni kwenda nje ya hapo tuupate ukweli
 
Ni bora mara mia VP akapewa mwijaku au steve nyerere.
 
Hatokusikiliza. Ni mtu anayeamini wengine sie ni wajinga flani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…