Nawashukuru Watanzania-Waasia hawa; historia itawakumbuka

Nahisi watanzania wenye uwezo wa kumwaga "ugali" ni wachache sana. Kumbuka asilimia si chini ya 70 ya watanzania wapo vijijini na hii ripoti sidhani kama wameisikia.
 
Nahisi watanzania wenye uwezo wa kumwaga "ugali" ni wachache sana. Kumbuka asilimia si chini ya 70 ya watanzania wapo vijijini na hii ripoti sidhani kama wameisikia.


Usijali Mungu si Athumani kama walivyo mwaga mboga hao ambao hawakutegemewa ndivyo itakavyo kuwa kwa watakao mwaga ugali. Hakuna mfumo wa kibinadamu wa kidhalimu utakao dumu milele....time is a gudi furendi...
 
Uzushi mtupu, gari moshi lilianzia stesheni namba moja, chanzo cha matatizo yote ya Tanzania ya leo ni Nyerere, Ujamaa ulikuwa ni chanzo cha matatizo na hilo halipingiki.
"[FONT=Verdana,Arial,Helvetica]But the Tanzanian experiment offers good evidence that saints do not really make very good presidents"[/FONT]


Kaka/Dada hebu pitia kidogo JF Doctor ukapate ushauri maana lazima utakuwa unaumwa "something"..........
 
WABAKAJI WA UCHUMI DUNIANI WANAJUA NAMNA YA KUWATUMIA HAWA WAZEE VILAZA MA-MBUMBUMBUU WASIO NA UWEZO WA KUFIKIRI UREFU WA PUA YAO...

WANAJUA KUWA UCHAGUZI FEKI = RAIS FEKI + MAWAZIRI FEKI + WABUNGE FEKI + MAJAJI FEKI + MAJESHI FEKI + MABENKI FEKI + KILIMO FEKI + UVUVI FEKI + UFUGAJI FEKI + SEKTA YA MADINI FEKI + MIPANGO FEKI + VIWANDA FEKI + MASHIRIKA FEKI + VYUO FEKI + HOSPITALI FEKI + MIUNDO MBINU FEKI + MAKANISA FEKI + MISIKITI FEKI + WAUMINI FEKI + WANANCHI FEKI + FIKRA FEKI + MISHAHARA FEKI + WAZALENDO FEKI
= WATAWALIWA MILELE !!! KUDOS MWANAKIJIJI THO KAZI ZA MIKONO YAKO ITAKUJA KUONEKANA KWA VIZAZI VIJAVYO!!!
 
The evidence has been gathered from official
Bank of Tanzania documents, government agencies and authorities.

Kama tungo hii ni kweli basi,
1. Hata Watanzania wenye asili ya Afrika wanaweza kuwa ndio wengi wamehusika kuzinyofoa hizo 'primary' data na kuwakabidhi hao waliozikusanya (gather) na kuziwasilisha maana ndio watumishi wengi walioko kwenye Mabenki na Asasi / Wakala wa Serikali.
2. Hata UWT nao wanaweza kuwa wamehusika maana nao ni sehemu ya Asasi / Mamlaka za Serikali na hata humo wahusika wanaweza kuwa wenye asili ya Kiafrika na Kiasia au asili nyinginezo (nani anasema UWT haina maajenti wenye asili tofauti na ya Kiafrika?).

BTW.
Mwanakijiji, waliokusanya (gather) data unasema ni wa asili ya Asia, je waliozipanga, kuzichambua na kuzitafsiri (organise, analyze & interpret) walikuwa wenye asili gani maana hao nao ni muhimu sana.
Aidha binafsi nina swali juu ya hiyo organogram ya Umafia wao; kwamba ni kwa nini JayantKumar Patel (Alias Jeetu Patel) ndiye aitwe Head of Crime Family? Je ni kwa sababu ndiye aliyefaidika sana na mfumo, au ndiye kweli kiongozi mfawidi wa ufisadi 'wooote' huo yaani anayetengeneza sera na au kutoa amri nini kifanyike kote huko au ni kwa sababu ndiye mwenye makosa ya jinai kibao katika nchi yetu na nje kuliko hao wengine. Je kweli muundo (organisation structure) wa Umafia wao ni wa msoge kama unavyoonekana au ni wa style ya mtando wa buibui. Na je yeye mwenyewe huko juu kabisa ANAWAJIBIKA KWA NANI? (yaani uki- extrapolate lines of authorities juu ya Jeetu Patel kuna nani au kuna asasi gani au yeye ndiyo mwanzo na mwisho kama Mungu?

Zaidi ya pongezi kwa KUKUSANYA (GATHERING), mimi natoa pongezi za dhati za ukabla (in advance) kwa wote wenye asili yeyote WATAKAOZITUMIA (UTILIZATION) takwimu au taarifa za kweli na zilizo kamili kwa ajili ya maendeleo ya nchi na dunia kwa ujumla.

Mwalimu wangu alisema, ' Data are like bikinis. What they reveal is suggestive, but what they conceal is vital'
 
Umenikumbusha maneno ya mzee ruksa...zamani zilee alisema: kosa la pateli ni la pateli peke yake na si la wahindi wote...na kosa la masanja ni la masanja pekee si la wasukuma wote...hii imethibitisha kuwa kumbe kuna waasia wengine si magabachori. mzee mwanakijiji ahsante sana kwa kutufungua macho.
 
Historia itawakumbuka sana hawa watanzania wenye asili ya Asia.
 
hata kama hawakutajwa wanajijua pongezi ziwaendee popote mlipo
 

Lakini tukumbuke kwamba hawa waasia walimwaga mboga baada ya wao kukosa "mnuso" hapo BoT. Nia hasa ilikuwa ni kukomoana. Ndio maana hata Rais alipohutubia Bunge Agosti 2008 huko Dodoma alisema "bila ugonvi wa wafanyabiashara sakata la EPA lisingejulikana kwa umma". Binafsi namshukuru IBILISI aliyewafanya hawa waasia wagombane wao kwa wao. Wangechotewa EPA wasingetoboa siri hata kidogo. Ndio mana hata Gavana Bilali alivyopewa hiyo ripoti kwa mara ya kwanza na kuisoma alijisahau na kubwatuka mbele ya msaidizi wake akasema "huyu ni ......". Alimjua kwa vile alijua kwamba alimkatalia ombi lake la kuchota EPA.

Waasia ni waasia tu. wana mwili (makazi) wao Tanzania, roho yao iko India na Pesa yao Canada au Ulaya.
 
Kazi ipo. Naisubiri kama wewe, Mama Sophia S na wengine tele ambao either majuzi, juzi au jana na pengine leo wameamua kuwa wapiganaji tunavyoisubiri
Project X-201
0
In initiating stage...
"Change is coming; be part of it, don't wait for it"!

Well, kwa wale ambao hawajui ninazungumzia nini, nimeiambatanisha.[/QUOTE]
 

Sidhani kama hawa jamaa ndio waliotia funguo gari moshi.... noo hapana! Unamkumbuka mwandishi Stan katabalo na kashfa ya Loliondo?


Mwizi aliyesalitiwa na wenziwe akaamua kuwachoma leo hii tumshukuru na kumuona shujaa mpaka historia imkumbuke kweli...!!!!?
 
kitu cha kushangaza ni mfano serikali ilitahadhalishwa mapema kuhusu RITES ya India lakini waziri akang'ang'ana kwamba lazima waingie mkataba na hiyo kampuni. Je sasa hivi kwa nini aliye saini mkataba asifungwe??

Hapo ndo mimi sina imani na JK kabisa.
 

Mkuu Byasel,
Nakubaliana na maoni yako 100% kwa ufahamu nilio nao. Na pia ili tusifanye dhambi kama yupo ambaye kweli alifanya hayo kwa kuwa mzalendo wa kweli basi anastahili sifa na hizo asante, I really doubt there is.... but that space should be provided and be there!
Kinachonishangaza baadhi ya watajwa kwenye hizi scandle bado wanafanya biashara kubwa tu hapo dar na watu hawana habari tunakwenda kutaka kufanya nao bishara kubwa tu!! Thkis has truly shocked me, sasa hii serikali hata haijali inawaachia wazidi kutumaliza nini? Kuna jamaa yangu alitaka kununua nyumba kwa mmoja wao ya thamani ya zaidi ya Tshs.130mln watu wa benki ndiyo walimshangaza walipokataa kupeleka fedha kwenye akaunti ya hiyo kampuni. Hii si ni hatari sana? Kwanini serikali imekaa pembeni inaangalia?? Aggrrrrr!
 
Hivi ka-inzi kana rangi au kabila?
Alaa mkuu huna bahari kuna nzi wa rangi ya blu makazi yao ktk chimoni, hawajishughulishi na mabaki ya embe ..wao wanajua fika kwamba uchafu wa binadamu huishia shimoni ambako ndiko kuna ulaji wa kupumzika na sii mabaki ya mifupa wanayokimbilia walalahoi (nzi wa kijivu) ambao kila siku wanaepa mikono ya binadamu..
 

...duuh.....Mkuu unaweza kutupa tafsiri yake kwa Kikerewe?
 
Ogah,
Haaa! haaa! haaa! Kikerewe kipi - Kisilanga au Kiruhu?..
Ni hivi hawa wadosti sii wenzetu, yaani sii nzi wa kijivu (kama sisi) ambao utawaona wakizengea zengea wakisha nusa harufu ya chakula..
hawa hupenda harufu (Ufisadi) sehemu ambazo wewe na mimi hatuwezi kwenda wala kujaribu kuvuta mnuso wa BoT.
Hivyo, tuwape sifa zao kama alivyosema Mwanakijiji, Ni watanzania na bila shaka hilo neno waasia kaliweka makusudi kutofautisha na wengine ambao hawatoki msalani wanazengea ukija chuchumaa tu wanaanza makamuzi...
Haaa! haaa! haaa!
 
Ukubali au ukatae, upende au usipende, hii inchi inamilikiwa na Waasia.
 

Mbona umewasahau Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…