Nawashwa mwilini mzima

Nawashwa mwilini mzima

Davidson david

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2023
Posts
1,029
Reaction score
1,051
Jamani natatizo la kuwashwa zaid miez 10 nmetumia dawa za allergy cream za fungus lakini sponi
 
Umetoka vipele?

Muda mwingine sio lazima daktari,

We angalia km kuna mafuta mapya, au sabuni au chakula miongoni mwa hivyo itakua ndio chanzo,

Ikiwa ni hivyo hata upewe dawa gani, hutapona mana bado inayosababisha allergy unaitumia, DO A SELF EXAMINATION AND ANALYSIS
 
Kuna siku nilienda hospitali flani hivi nikahitaji nionane na daktari wa kiume kwa sababu ya tatizo lililokuwa linanisumbua kwa wakati huo.

Basi wakani direct moja kwa moja kwa mzee mmoja hv aliyekuwa daktari katika ile hospitali nikamuelezea kuhusu matatizo ya ngozi yaliyokuwa yananisumbua na yaliyoambatana na muwasho mkubwa uliokuwa ni adha kubwa kwangu.

Basi alichonishauri cha kwanza ilikuwa ni kuhusu usafi.


USAFI USAFI USAFI.

alinisisitizia nioge tena kwa maji ambayo ni mengi.

Mtu mzima nenda kaoge na ndoo ya lita 20 sio kale ka lita 10.

Lakini pia akaniambia hakikisha unadumisha usafi japo alinipa dawa.

Ila naamini ule ushauri ulinisaidia kwa kiasi kikubwa.


Kama una magonjwa ya ngozi miongoni mwa silaha kubwa, unapokuwa unatumia tiba basi dumisha usafi wa mwili.

Naamini hata uponaji wake utakuwa ni wa haraka.
 
Jamani natatizo la kuwashwa zaid miez 10 nmetumia dawa za allergy cream za fungus lakini sponi
Unaogea sabuni gani ya mche, ya unga, ya ngozi, ya marashi, ya kemikali, ya kujichubua ngozi?

Unatumia mafuta gani ya nazi, ya mgando, ya lotion, ya kemikali?

Unafua nguo zako mara kwa mara au unajivundika mpaka unachacha maa na nguo hizo hizo Mwezi mzima?

Unaoga mara ngapi kwa siku, mara 1, mara 2 au mara 3?

Unavaliana nguo na mtu yeyote, ndio au hapana?

Mara ya mwisho kuhudhuria hospital ilikua lini na vipimo vilionyesha unasumbuliwa na nini?

Ushawahi mtembelea specialist yoyote WA magonjwa ya ngozi, mara ya mwisho kuonana na specialist ilikua lini?

Tupatie hayo majibu alafu Madaktari wa JF tukusaidie zaidi
 
Back
Top Bottom