Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Wengi tuliamini Jeshi la Polisi linahusika Kuteka na kutesa watu hasa Wenye kukosoa serikali katika Mambo mbalimbali. Lakini Jana IGP CAMILIUS WAMBURA akiwa Bariadi ameta.ka Wazi kabisa Polisi wake hawahusiki. Na ametoa mifano ya Mtoto wa Mbeya aliyetekwa Kwa maelekezo ya mama yake ili apate hela toka Kwa mzazi mwenzie na watoto wawili wa Mwanza mkubwa akiwa na miaka 12 waliojiteka na kupanga chumba ili wapige hela Kwa mama yao mzazi lakini Kwa weledi wa hali ya juu kabisa Polisi wa Bwana Wambura wakategua mtego ule na kuwakamata.
Baada ya yeye kutoa mifano na Mimi naomba nitoe mifano ya waliojiteka na kuwasihi Vijana wengine hili liwe fundisho kwao wakome kujiteka kama hawa nitakaowatolea mifano. WA Kwanza ni huyu shujaa wa Twitter X SATIVA aliyejiteka Kimara DSM, kisha Kwa utundu wake akajipeleka Polisi Oesterbay kwenye karakana akajipigapiga na vyuma vya magari kisha akaokota Pingu iliyosahauliwa na Askari wa traffic aliyekuwa amemfunga dereva wa daladala iliyopata ajali na kujifunga mikononi kisha akapanda basi la Air Msae Hadi Arusha Kwa demu wake ambako alikaa siku 2 na baadaye akapanda AN bus Hadi Katavi ambako alijipiga risasi ya taya Kwa bunduki aliyoachiwa na Marehemu Baba yake. Huyu bila wasamalia wema waliomuokota angekufa Kwa "ujinga" wake porini.
Pia soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Wa pili ni Mombo kijana toka Handeni Tanga. Mgosi huyu naye kaleta usanii wa kisambaa. Kajiteka Tangu June 14 usiku kaenda kwenye mashamba ya Mapeas huko kajiburuza wewe kisha Kwa ujanja ujanja akajipenyeza Hadi lock up ya Polisi Handeni na kujichanganya na washtamiwa Ili ionekane alikamatwa na Polisi. Kumbe Polisi wa watu wala hawakuwa na shida naye japokuwa kuna kipindi zamaaani waliwahi kumtafuta Kwa makosa yake ya kuandika vitaarifa vya kishakunaku mitandaoni lakini walikuwa hawamtafuti kiviiile.
Sasa Kwa mifano hii miwili niungane na Jeshi tukufu la Polisi kukemea Tabia hii ya kujiteka iliyofanywa na Vijana hawa wawili Kwa lengo la kuchafua sifa nzuri ya Nchi yetu ya Amani na utulivu. Nawaunga mkono Polisi SATIVA na Mombo wafikishwe mahakamani Kwa kosa la kujiteka ili liwe fundisho Kwa Vijana wengine.