Nawatafuta ndugu wa baba yangu

whitemoney

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2023
Posts
1,161
Reaction score
2,454
Nilizaliwa Simanjiro. Baba alifariki nikiwa bado mdogo (mwaka 2003), na bahati mbaya mama naye alifariki mwaka 2005. Sina ndugu yoyote wa kuzaliwa tumbo moja, labda ingekuwa afadhali.

Mama aliwahi kunieleza kuwa baba alikuwa mzaliwa wa Nachingwea, Lindi, na alifahamika kwa jina la Yahaya Tilika. Sifahamu hata ndugu mmoja wa upande wa baba.

Ingawa sasa nimekuwa mtu mzima na nimeshavuka changamoto nyingi kivyangu, bado ninahitaji kuwapata baba wakubwa/wadogo zangu na mashangazi. Nina imani wapo.

JF Forum ni kubwa na inatukutanisha na watu wenye mawazo tofauti. Kama kuna mtu mwenye ufahamu au mchango wowote wa namna ya kuwapata, tafadhali naomba msaada wako.

Mawasiliano: 0686633597
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…