Nawatakia kheri kidato cha nne, 2014

Nawatakia kheri kidato cha nne, 2014

katika mitihani hii kila mtu atavuna alichopanda. kama mtu ulipanda bangi usitegemee kuvuna mchicha. ni wakati mwingine tena tutegemee kuwaona wanafunzi wakiandika matusi na kumchora messi kwenye karatasi zao za majibu.
 
Tutapata ma barmaid wa kutosha na wanenguaji wa kutosha.
Mwenye busara huongea inapobidi lakini mjinga huongea ilimradi! Akili yako finyu sana. Wewe unadhani barmaid sio watu muhimu na wanenguaji(wasanii) sio watu muhimu?! Kila mtu na kazi yake na tuwape heshima watu watu wanaotafuta riziki zao kihalali. Wanenguaji ni kama hao akina Diamond na Lina. Hao ni wasanii wenye mafanikio sana katika kazi zao na inawezekana wanapesa kuliko hata wewe kwa kazi hizo hizo ambazo wewe unazidharau. Imagine umeenda bar halafu ukute hakuna wahudumu utajisikiaje? Kila kazi inahitaji watu na lazima tujifunze kuheshimu watu na kazi zao kwani wewe hata kama una kazi nzuri haiwasadii wao. Wewe unaonekana kuwa na mawazo ya hovyo kabisa!
 
Mtu mzima inatakiwa kuwa na busara kwenye vitu vya maana sio unakurupuka kutoka chooni halafu unacomment, utacomment upuuzi kama ulioufanya, watoto wako ndio watakuwa barmaid na wacheza shoo, mungu awabariki wote mnaofanya mitihani ya kidato cha 4, mungu awabariki muanze salama mmalize salama,amen.
Well said mkuu Nimeona reaction zake kwako anaonekana hana akili nzuri. Achana nae atakuharibia siku huyo. Huyo bwana kama ni mtu mzima anaonekana atakuwa mtu mzima hovyo kabisa! Anaongea hovyo(anatukana) na sijui mods kama wako macho au wamelala
 
Mbona mimi naona ni mda sana kaka, hapa nilipo ni baba wa watoto 4. Nenda kule kwenye jukwaa la MMU, CHIT CHAT NA CELEBRITIES usishangae kuna watoto wa FORM 3 KAKA.

2007 na una watoto wanne! Naona umewahi sn mkuu labda km ni mapacha. Mi nilimaliza 2005 na ndio kwanza nina mtoto mmoja.
 
Kila la kheri wadogo zangu,Mwenyezi Mungu awatangulie kwenye mitihani yenu.
 
2007 na una watoto wanne! Naona umewahi sn mkuu labda km ni mapacha. Mi nilimaliza 2005 na ndio kwanza nina mtoto mmoja.

Wapo mapacha, wa kwanza wamezaliwa 28/04/2012 na wengind wamezaliwa ijumaa iliyopita.
 
Kila laheri vijana wetu. Karibuni mtaani mwonje ladha ya maisha.
 
Mwenyenzi Mungu baba wa amani katika jina la Yesu Kristo twawakabidhi vijana wa kidato cha nne wafanye mitihani yao kwa amani, uwape utulivu wa akili na mawazo yao, uwaondolee hofu na kutojiamini. Hila zote za mwovu shetani zikashindwe katika jina la Yesu. Wafaulu na kuja kulitumikia taifa lao kwa moyo wa dhati na uzalendo wa hali ya juu. Amen!
 
Mwenye busara huongea inapobidi lakini mjinga huongea ilimradi! Akili yako finyu sana. Wewe unadhani barmaid sio watu muhimu na wanenguaji(wasanii) sio watu muhimu?! Kila mtu na kazi yake na tuwape heshima watu watu wanaotafuta riziki zao kihalali. Wanenguaji ni kama hao akina Diamond na Lina. Hao ni wasanii wenye mafanikio sana katika kazi zao na inawezekana wanapesa kuliko hata wewe kwa kazi hizo hizo ambazo wewe unazidharau. Imagine umeenda bar halafu ukute hakuna wahudumu utajisikiaje? Kila kazi inahitaji watu na lazima tujifunze kuheshimu watu na kazi zao kwani wewe hata kama una kazi nzuri haiwasadii wao. Wewe unaonekana kuwa na mawazo ya hovyo kabisa!
sawa mhudumu
 
Back
Top Bottom