Nawatakia waadventista wasabato na waumini wa dini ya kiyahudi siku ya mapumziko (sabato), Tuendelee kutii amri kumi bila ubaguzi

Ahsante,barikiwe.
 
Wasabato wanaamini mafundisho yaliyotolewa na Ellen G White kuliko yaliyomo kwenye Biblia na hili ni tatizo kubwa. Kwa msabato mafundisho ya Biblia yakipishana na maono ya Ellen G White basi ya Ellen yatapewa kipaumbele na ya Bible yatapewa Back seat. Wasabato wengi hawajui hili ila ndo iko hivyo.
 
1 Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.
2 Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
3 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?
4 jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?
5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?
6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.
7 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.
8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
 
Ni adhabu gani Mtu alistahili kupewa au atapewa Kwa kutoshika sabato?
Ni mtu ambae hata hajali mapumziko ya wafanyakazi wake ama mifugo yake,

Adhabu kibao zinamsubiri, mojawapo haina tofauti na mtu muonezi
 
Mafundishho yote ya Ellen G White yana reference kwenye biblia.

Hata Mwakasege naye ni mwalimu, Reference zake ni kwenye biblia, anasihi tusizini kwa reference ya biblia, tusiwe wezi kwa reference ya biblia, n,k.
 
Mungu alifanya kazi siku sita akamaliza ndipo akapumzika wewe unapumzika umemaliza kazi zako
 
Mungu alifanya kazi siku sita akamaliza ndipo akapumzika wewe unapumzika umemaliza kazi zako
Siku ya sabato Ina rangi gani, au Ina alama gani kuwa ni sabato , mfano Mimi nikiamua jumatano ndo siku yangu ya mapumziko. Kumbuka hizo siku na majina ni sisi binadamu tulipanga
 
Yesu kajiita mwana wa adamu (Son of man) zaidi ya mara 30, hivyo akimaanisha kwamba kuiabudu sabato ni kumuabudu na yeye.

Mafarisayo walianzisha sheria zao zilizofanya sabato ionekane kama utumwa ikiwemo kukataza kula bila kuosha mikono kwa mitindo yao, kukataza kuokoa mifugo siku ya sabato, n.k. Yesu alikuja kuieka sawa, Marko 2:27-28 "Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato."
 
Ni mtu ambae hata hajali mapumziko ya wafanyakazi wake ama mifugo yake,

Adhabu kibao zinamsubiri, mojawapo haina tofauti na mtu muonezi
Basi hiyo unayoshika wewe siyo sabato ya Musa...Ni wewe tu umechagua kupumzika jumamosi

Ile ya Musa ilikuwa ni Lazima na adhabu ilitolewa Kwa waisraeli wasiotii mpaka siku za Yesu ilikuwa hivyo Ila sasa ni tofauti na hiyo


Kutoka 31:14 Ni lazima mshike Sabato kwa sababu ni takatifu kwenu. Mtu yeyote atakayeitia unajisi ni lazima auawe. Mtu yeyote atakayefanya kazi siku hiyo, ni lazima auawe kutoka kati ya watu wake.
 
Mafundishho yote ya Ellen G White yana reference kwenye biblia.

Hata Mwakasege naye ni mwalimu, Reference zake ni kwenye biblia, anasihi tusizini kwa reference ya biblia, tusiwe wezi kwa reference ya biblia, n,k.
Na wale waliotaka kusafiri kwenda France bila Passport wala tiketi ni kifungu gani?
 
Lakini Sabato siyo hii JUMAMOSI kama kesho
 
Ni jambo jema kukumbuka/kumbushana kumuabudu aliyetuumba.

Ujumbe mzuri mwenye wito auitike.
 
Mungu alifanya kazi siku sita akamaliza ndipo akapumzika wewe unapumzika umemaliza kazi zako
Ni kusema ataenda kupumzika kaburini?

Utakuta nae kufa hataki ili akapate hilo pumziko aisee mbingu siyo kitu cha mchezo mchezo kama kweli ipo mpaka sasa itabidi Mungu awe amebadili baadhi ya mambo maana kwa dunia ya leo na yanayoendelea hatapata wa kuingia humo wote motoni.
 
Kwa enzi hizo adhabu za kuvunja amri 10 za Mungu zilikuwa na adhabu kali mnoo na instant !! ikiwemo hata hio ya kuto abudu siku ya sabato.

Kwa sasa mambo yamebadilika, Tunapewa hata nafasi ya kuwezo kutubu bila kutoa kafara za wanyama bali kutumia damu ya Yesu popote pale.

Lakini haimaanishi kwamba tuache kuzifuata amri 10 ikiwemo kuiabudu siku ya sabato.
 
Basi tunakubaliana Sheria imebadilika kutia Ndani maagizo ya sabato Ile waisraeli walishika hii ni tofauti maana haitii maagizo yote ya Musa😊

Hilo Lina maana Sana na ndio Jambo kuu kapitie tena kitabu cha waebrania
 
Sawa. Sasa mwinjilisti Musa alipotoka kule mlimani na zile Amri 10 mbona hakuwapa makabila mengine yaliyokuwepo mengi tu kuwaambia washike sabato. Aliwaambia Waisrael tu.
Sabato ni kwa wayahudi tu

Kama na wewe unataks kushika sabato basi ka nayo wewe, kuwahubiria wenzako unapoteza Muda.

Ndio maana Mtume Paulo alikuwa anahubiri injili na Timoteo ambae ana govi hajatahiriwa kama maagizo ya package ya maagano ikiwemo Amri 10.
Alimtahiri kuwafurahisha tu wayahudi.
Kidogp kidogo utaelewa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…