VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kila linapoletwa ubaoni na mezani suala la Katiba mpya, wanaCCM huwa mbele kuvuruga kwa kelele kupiga. Katiba ya sasa ya Tanzania iliandikwa mwaka 1977, takribani miaka 44 iliyopita. Katiba hiyo imeshafanyiwa mabadiliko mbalimbali zaidi ya kumi. Ndiyo kusema bila kuhema kuwa Katiba ya sasa ina viraka na mabaka ya uhakika.
Mwaka 2014, Rais na Mwenyekiti Mstaafu Kikwete alianzisha na kuusimamia mchakato wa Katiba mpya. Akampa wajibu mujarabu wa kutafuta jibu la kikatiba kaka yangu Jaji Joseph Sinde Warioba na Tume yake. Hata Bunge la Katiba liliundwa lakini likashindwa.
Kule kwenye Bunge la Katiba, CCM liliuteka mchakato na kuuvuruga bila uoga. Mchakato ukafia kwenye Katiba Pendekezwa ambayo hadi leo haijawahi kuendelezwa wala kuzungumzwa. Kila kiongozi anayeshika madaraka, tena kwa haraka, husema kuwa Katiba mpya si ajenda yake.
Hivi sasa CHADEMA na wapendakatibampya wengine wameanzisha vuguvugu lisilo na vurugu la kutaka Katiba mpya. Vuguvugu hilo linakutana na mkono wa chuma usio na huruma kutoka Serikalini na chamani-CCM ili likwame kama kuzimika kwa umeme. Tayari mamia wamekamatwa na/au kushtakiwa kwa makosa mazitomazito na ya kuogofya.
Kwanini CCM na Serikali yetu tunaikataa na kuichukia Katiba mpya kiasi hiki? Kuupenda Mwenge wa Uhuru na kuung'ang'ania kwa miaka yote hiyo si mfano wa kubaki na Katiba ya sasa. Katiba ya sasa ina mapungufu mengi. Ina maswali mengi kuliko majibu. Katiba mpya ni jambo jema. Haipaswi kuchukiwa na kupingwa kwa kiasi hiki. CCM tubadilike.
IGP Sirro, kwanini umezungumzia kesi ya Mbowe iliyopo Mahakamani?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam