Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwanza naomba kukiri kwamba mimi ni Mwanasimba ( mmoja wa wachangiaji wa hela za kuendesha timu ) , ambaye sijaridhishwa na mchakato wa kumuuzia hisa za Simba mtu ambaye anayo historia ya wazi ya kushindwa .
Mohamed Dewji aliwahi kumiliki timu ya soka ambayo baadaye ilishuka daraja , hakuna aliyesahau hili , kama timu aliyoimilki kwa 100% iliporomoka , vipi hii 49% ? , kingine ni kwamba , huyu alikuwa mfadhili wa Singida United alipokuwa mbunge , kipi ilichofanikiwa timu ile , mbona ilishuka daraja na kupotea ? Shukrani kwa walioirejesha tena ligi kuu .
Kwenye mchakato wa kummilikisha hisa za Simba alishindanishwa na nani , yeye alipata kura ngapi na huyo mwengine alipata ngapi ? Tunauliza hivi ili baadaye msije kushikana mashati .
Majuto ni mjukuu .