goshaiwedi
Member
- Feb 23, 2020
- 60
- 76
Ndugu zangu watajwa hapo juu, nyie ni nyota katika tasnia ya mpira hapa Tanzania na inawezekana yaliyotokea hapo nyuma yaliwafanya mkafikia maamuzi mliyofikia lakini kila nikitizama naona iko haja ya kujitafakari upya, hapo mlipo yaani Simba SC ni ukweli usiokanika kuwa hamna namba katika kikosi cha kwanza, na ni ukweli kuwa bado viwango vyenu viko juu ila kinachowaponza ni kukosa namba kutokana na ushindani uliopo hapo Simba.
Ushauri wangu kwako Gadiel Maiko na Ajib rudini kundini au tafuteni timu mtakayopata nafasi ya kucheza mara kwa mara,tofauti na hivyo mjue mnapotea katika ulimwengu wa soka.
Nendeni hata Polisi, Kagera, Mtibwa n.k ili mradi mpate nafasi, kuitwa mchezaji wa simba au Yanga wakati huna nafasi ni undondocha.
Sent using Jamii Forums mobile app