Nawaza kimaandishi: helkopta zitakuwa kama bodaboda!

Nawaza kimaandishi: helkopta zitakuwa kama bodaboda!

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
906
Reaction score
426
Wachina walipotengeneza pikipiki zao za mwanzo, (SanLG na Toyo) ziliingia soko la Tanzania kwa bei ya shilingi laki nne tu. Mchina alipoanza kuuza pikipiki zake kwa laki nne pikipiki ya Mjapan aina ya Honda 110 ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi milioni sita hadi 10!. Kabla ya kuja kwa SanLG na Toyo; pikipiki ilionekana ni chombo cha wenye nazo! Wajasiriamali waliochangamkia fursa ya pikipiki za Toyo pale mwanzo kabisa kwa kuzifanya bodaboda; walitengeneza “Faida kubwa sana””.

Baada ya kuona Wachina wanakimbiza sokoni; Wahindi na Wajapan nao wakasalimu amri nao wakaanza kutengeneza pikipiki za bei ndogo. Kwa kutumia mfano huo; natafakari fursa ya usafiri wa anga. Hivi sasa Helkopta ya kawaida ikiwa mpya (yenye siti 5-Robbinson R26) inauzwa kwa tsh Bilioni 1.5. Wajasiriamali wanaoweza kumudu gharama hii ni wachache. Lakini ni nani ajuaye ikiwa Wachina hawaumizi vichwa kutengeneza Helkopta za ‘ki-SanLG’ ama za ‘ki-Toyo?’ Kwa mahesabu ya “kipikipiki”, ikiwa “Wachina” watafanikiwa kutuundia Helkopta za ‘Ki-SanLG’, helkopta itauzwa kwa tsh Milioni 100 tu! Na hata kama huviamini vitu vya Kichina, usijali; kwa sababu nina uhakika kuwa Wahindi, Wajapan na wengine(unaowaamini) watafuata nyayo za Mchina kutengeneza helkopta za bei nafuu.

Opsiii; ikifika hapo bila shaka wajasiriamali wengi (na watu wengine) watazichangamkia na zitakuwa nyingi kama boda-boda. Najua unaweza kuona kuwa ni jambo gumu,-upo sahihi; kwani hata enzi za pikipiki za Honda wengi waliona isingewezekana vijiji vyote Tanzania kufurika pikipiki.

Tena hakuna aliyedhani ikiwa serikali ingehalalisha usafiri wa bodaboda kwa kutoa leseni. Kwa kuwa helkopta zinatua popote; basi wajasiriamali watakaowahi kununua mapema hizo helkopta naamini watatengeneza”Faida kubwa sana”. Maombi yangu kwa Mungu ni kwamba, kama ambavyo wengi wananunua bodaboda siku hizi; mimi na wewe tukawe miongoni mwao walio wengi watakaomudu kununua helkopta siku si nyingi zijazo; hilo likatokee kwako na kwangu; iwe bei ya helkopta itashuka ama itapanda, vyovyote vile; tukamiliki.

Hata kama kilichotokea kwa bodaboda kisipotokea kwa helkopta, kwamba helkopta zikabaki kuwa za “mabilionea”, mimi bado nakuombea uje uimiliki. Usiiogope milioni 100, wala usijidharau usikiapo bilioni 1.5, wewe sema, Amen, ikiwa unaamini kwamba kesho utakuwa “matawi” ya juu kuliko ulivyo leo!
5cc5dc3d881f9b8a4682e47e159702d7.jpg
 
Back
Top Bottom