Nawaza kitakachotokea ziara ya Kamala Harris

Nawaza kitakachotokea ziara ya Kamala Harris

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Atamsifia Samia kwamba kaimarisha demokrasia na kwamba kaleta haki za binadamu na karuhusu upinzani kufanya mikutano. Samia atavimba kichwa na kufurahi kusifiwa na makamu wa rais wa Marekani kumbe wananchi shida yao ni uchumi. Kamalla atapiga vijembe awamu ya tano na kujidai hali ya Tanzania sasa ni nzuri.

Kamala Atatangaza misaada ambayo ukichunguza in substance hela zinaenda kuliwa tu na vigogo tu. Ni kama anakuja kutoa rushwa kwa viongozi wetu.

Utasikia dola laki kadhaa kuimarisha ufuatiliaji wa usimamizi wa utafiti kuhusu kuimarisha umeme nchini. Hapo hola hakuna kitu. Hela za night safari za Ulaya na kulipia mahoteli. Vigogo tu ndio wanakula misaada ya wamarekani. Hapo bado component ya washauri kutoka Marekani.

Kila la kheri ushirikiano wa Samia na kamala Harris😆😎
 
Na pia mara kadhaa kwenye kura za UN kuhusu russia, Tz imekuwa ikikaa kimya baada ya hii ziara si ajabu tukaona tz inasupport resolution za UN against Russia. Au kuna deal la madini linatafutwa
 
USA akupende halafu iweje, maendeleo hayaletwi kwa msaada wa kodi za watu wengine.

Maendeleo yanaletwa kwa watu wa Taifa husika kufanya kazi kwa bidii, kulinda misingi na kuheshimiana.
 
Na pia mara kadhaa kwenye kura za UN kuhusu russia, Tz imekuwa ikikaa kimya baada ya hii ziara si ajabu tukaona tz inasupport resolution za UN against Russia. Au kuna deal la madini linatafutwa
Tukiingia kwenye huo mtego, basi na kale "KABIASHARA" kengine tutaingia kama kina OMERA...
 
Tukiingia kwenye huo mtego, basi na kale "KABIASHARA" kengine tutaingia kama kina OMERA...
kwa ziara za ghafla namna hii tutaingia tu...ukiangalia nchi anazotembelea zambia, TZ na ghana(nadhani) ni nchi zenye utulivu ambazo china ina influence fulani....na china uko damudamu na urusi
 
Back
Top Bottom