Nawaza kwa sauti ikiwa huu ndio mkakati wa UPINZANI" Kumnanga Magufuli halafu 2025 kumtumia kwenye kampeni"

Nawaza kwa sauti ikiwa huu ndio mkakati wa UPINZANI" Kumnanga Magufuli halafu 2025 kumtumia kwenye kampeni"

FPT

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,216
Reaction score
1,848
Moja ya mkakati unaotumiwa sana ni kutumia njia ya kujiweka mbali ili adui yako hasikufikirie zaidi. Na kwa ujumla mkakati huu nawaza pengine unatumiwa na vyama vya upinzani kuizubaisha CCM wanavyomchukulia Hayati Magufuli. Kama ndivyo basi CCM.

Machoni mwa wengi sana Hayati Magufuli ni shujaa anayeishi na pengine ndio ataamua Rais anayefata awe nani. Hivyo ni kitendo cha kusema turufu walizonazo wagombea iwe wa CCM au UPINZANI 2025 na 2030 ni JPM.

Sifirii kabisa Upinzani licha ya kutambua uwezo wa JPM katika kuamua matokeo katika chaguzi kuu zijazo wamedhamiria kumkebehi JPM bila kuwa na 'backup plan'.

Na hii ndio nafikiria ndio itakuwa 'backup plan' ya upinzani kwamba:

i) Kujifanya hawakumbali JPM
ii) Kuwaaminisha watanzania JPM si lolote si chochote.
iii) Kutumia majukwaa kumsema JPM ili CCM waamini.
iv) Baadae kumtumia JPM kama turufu muda ambao wengi hawataamini.

Kama huu ndio mpango wao basi hali itakuwa mbaya kwa CCM ikizingatiwa JPM anaonekana kwa wengi ni shujaa aliyefia vitani na upanga mkononi.
 
WAPINZANI baada ya kushindwa kumzima Magu mioyoni mwa Watanzania, wameamua kuungana na mafisadi.

Yaani mwanakondoo baada ya kuzidiwa na njaa, ameamua kwenda kunyonya matiti ya FISI 😳😳😳

NB; Maridhiano yenye TIJA ni KATIBA mpya na Si nusu mkate!!
 
Katika andiko lako umesahau kueleza kama anayonangwa Magufuli sio ya kweli. Kama ni ya kweli acha waendelee. Kwa sababu janga aliloleta Magu ni kubwa sana. Labda jiulize kwa nini historia zinaeleza kuhusu Idi Amini au Mobutu ili hali hawapo?

Halafu sidhani kama Chadema wakishika maiki ni Magufuli tuuu kuanzia asubuhi mpaka jioni, wanaeleza katiba mpya, wana bunge la wananchi, ugumu wa maisha nk. Magu alitia watu vilema,umasikini, kufarakanisha sasa usizuie victims kusema
 
Wauza ngada, wala rushwa, wavuvi,wanasiasa wa hovyo ndio waliomchukia Magufuli kwa wananchi wa kawaida alikuwa shujaa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wauza ngada, wala rushwa, wavuvi,wanasiasa wa hovyo ndio waliomchukia Magufuli kwa wananchi wa kawaida alikuwa shujaa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siasa za hovyo kama kuua watu bwa shee?Huwezi kutetea muuaji Kwa kisingizio cha rushwa au ufisadi.Huwezi kupambana na ufisadi au ngada bila kuua?Bora kafa.Saiz tunaishi Kwa amani sana bwa shee.Kama inakuuma jiue wewe sio kuua watu
 
Wauza ngada,wala rushwa, wavuvi,wanasiasa wa hovyo ndio waliomchukia Magufuli kwa wananchi wa kawaida alikuwa shujaa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Jadili acha kubwata na kubweka. Ukizungumzia rushwa Magufuli aliiba mpaka kuficha hela China. Haya sio maneno yangu ni ya Rais na CAG kataka uchunguzi. Ukizungumzia siasa za hovyo Magufuli ndio ticha. Aliwahi kusema hakupeleka maendeleo majimbo ya wapinzani kwa sababu ya kukosa connection.
 
Back
Top Bottom