Naweza kubadili jina nililotumia miaka mingi?

josephwaara

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2016
Posts
304
Reaction score
639
Wakuu heshima kwenu, naomba msaada katika suala hili.

Nilipofikisha umri wa miaka 10 niliugua sana, katika kutafuta tiba mzazi wangu akakutana na ushauri wa mimi kutumia jina jingne (nimefupisha story).

Sasa ishu hilo jina nikaja kusajiliwa nalo shule na kutumika kwenye vyeti vyote vya shule na cheti cha kuzaliwa. Hivyo ninafahamika kwa majina mawili tofauti kulingana na maeneo, sasa nimekuwa na nimepata mtoto na katika kumsajili nimetumia jina langu la awali ambalo linafanya sasa huyu mtoto aonekane siyo wangu kwa kuwa jina la baba ni tofauti.

Ninaweza kufanya nini ili niweze kumpatia bima ya afya? Solution ninayowaza ni mimi kubadili jina lirudi awali. Je itakuwaje wakati vyeti vyangu vyote vya taaluma na cha kuzaliwa vinasoma jina tofauti na lile la kuzaliwa?

Naomba mwongozo mkuu hili suala linantesa mno.
 
Nenda Rita Kule watakupa mwongozo. Ila nadhani lazima upite mahakamani uapishwe na hakimu kuwa majina yote ni ya kwako. Baada ya hapo Kule Rita wanafanya mabadiliko. Ila sasa:

1. Kwenye vyeti itabidi ufatilie upya upate vyeti vebye current name.

2. NIDA pia lazima upite.

3. Kwenye voters ID

Kama utaona kazi kubadilisha la kwako. Basi mtoto kama hujampatia cheti Cha kuzaliwa Inakuwa rahisi. Kama anacho inabidi upite mahakamani na Rita.

Ushauri mzuri ni kuwa badili ya mtoto kwako una vyeti vingi kazi itakuwa kubwa. .
 
Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.
Kwani siwezi kumiliki majina mawili??
 
Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.
Kwani siwezi kumiliki majina mawili??
Sasa unaweza kuwa na vitambulisho viwili?
Wengi wanaomiliki majina mawili unakuta Juma Hassan na jingine la ukol labda Juma Hassan kimweri. Hapo ndo unaweza miliki majina mawili. Nje ya hapo sijui. .
Kifupi unaweza kwenda RITA utapata maelekezo mazuri zaidi. .
 
Sawa mkuu ila shida yangu kubwa ni watoto kupata haki ya kutambulika kama mimi ni baba yao, ndo nawaza pengne lile jina lirasimishwe kama jina langu hata kama sitobadili hili la sasa.
Kwani siwezi kumiliki majina mawili??
Mkuu, kesho ndio "Last Seen/Comment" yangu humu jamiiforums. Tutaonana tena October 2024 (Miezi 23 kutoka mwezi huu).

Ninaangalia kwenye fursa nyingine ya pesa. Kwa bahati mbaya kwenye stories of change nimeangukia pua.

MAWASILIANO YANGU
===
Halotel - 0621 512 203 - Call/SMS

Tigo - 0654 527 779 - Call/SMS/Whatsapp
===

I wish you all the best.
 
josephwaara,

Kwanini lisibadlishwe la mtoto?

Leo unaongelea vitu vidogo TU kama bima ya afya!! Ulisha Kaa ukawaza Haki za huyo mtoto zilizoko hatarini Kutokana na huo mkanganyiko?

Jina lako kilibadili litakisumbua, maana limeisha enea sehem nyingi. Kwa vyovyite vile Kuna mahalo utanikuta mambo ya nagongana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnawapa tabu tu watoto kwa manufaa yenu binafsi.

Kadri miaka inavyozidi kwenda taarifa za mtu ni muhimu sana hasa majina yake na wazazi wake. Ikikosewa hata herufi tu huhesabika ni mtu mwingine hivyo huweza kukosa fursa adhim.

Nenda rita watakusaidia na kukupa mwongozo.
 
Dah yaani changamoto yako kama yangu asee
 
Kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto kuna sehemu ya kujaz jina la mtoto, andika andika jina lake kama linavyosomeka shuleni, sehemu ya jina la baba andika majina yako kama yanavyosomeka kwenye vyeti vyako. Mfano
Child's name: John Dowe Joseph
Father's name: JUMA SHAABANI HUSSEIN
Kwa maana hiyo tayar jina la baba limeonekana,
Chukulia mfano wale ambao huchukua ubini wa upande wa mama je majina ya baba zao huonekanaje kwenye chet cha kuzaliwa?
Kwa hiyo wewe nenda rita rekebisha namna hiyo.
Pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…