Naweza kupata tiba ya vidonge asilia kwa tatizo hili?

Joined
Mar 8, 2014
Posts
60
Reaction score
11
Wakuu naomba kuuliza kama kuna vidonge asilia vya kutibu tatizo kutosikia vizuri, kama tiba hiyo ipo ni wapi naweza kuipata kwa jijini Dar, na vipi gharama ya yake hadi kupona?na ni dozi ya muda gani?
 
Hali hio imeanza lini?una infection kwenye masikio?
Kama ni hali umezaliwa nayo nenda kwa daktari wa masikio ukafanyiwe uchunguzi masikio yako.
 
Kwa nini unaulizia vidonge vya tiba asilia?

Umeshajaribu matibabu ya hospitali ikashindikana?!
 
Kwa nini unaulizia vidonge vya tiba asilia?

Umeshajaribu matibabu ya hospitali ikashindikana?!

Mkuu kwa tatizo hili sijaenda hospitali ila nina hakika kuwa hospital hakuna tiba zaidi ya kukushauri ununue kifaa cha kuongeza kusikia.
 
Hali hio imeanza lini?una infection kwenye masikio?
Kama ni hali umezaliwa nayo nenda kwa daktari wa masikio ukafanyiwe uchunguzi masikio yako.

Hapana, imenianza kama miaka 10 iliyopita, awali tatizo lilikuwa kwa kiwango kidogo sana kiasi cha kwamba si rahisi kunijua nna tatizo, hata kwa sasa tatizo sio kubwa ila watu wanaweza kujua tatizo langu na kuniambia,
Kwahiyo naona ni bora nipate tiba kuliko kutumia kifaa cha kuongeza kusikia.
 
Usijipe uhakika. Nenda hospitali utashauriwa. Hizo tiba za jadi utaliwa tu hela zako. Mie nina mshkaji anavaa kifaa cha kusikia na yuko bomba tu, ni afisa wizara moja na ukatibu mkuu utamuangukia any minute. Usijinyanyapae bwana, nenda ukapate ushauri kwa ENT.
Mkuu kwa tatizo hili sijaenda hospitali ila nina hakika kuwa hospital hakuna tiba zaidi ya kukushauri ununue kifaa cha kuongeza kusikia.
 
Asante kwa ushauri wako, mimi sihitaji kuvaa hicho kifaa, kwani inasemwa kuwa kinaongeza tatizo na sio kutibu.
 
Mkuu naona umempa ushauri Mzuri. Yeye anakimbilia tiba za jadi wakati hajajua hata tatizo limesababishwa na nini!!
 
Wakuu naomba kuuliza kama kuna vidonge asilia vya kutibu tatizo kutosikia vizuri, kama tiba hiyo ipo ni wapi naweza kuipata kwa jijini Dar, na vipi gharama ya yake hadi kupona?na ni dozi ya muda gani?
Kuna mtalaam mmoja yupo mjini Pemba anaweza kukusaidia kukutibia hayo matatizo ya kutosikia vizuri ngoja nitafute Contact zake nitakujuulisha inshallah
 
Cc: MziziMkavu King'asti & co.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…