Health service
Member
- Mar 8, 2014
- 60
- 11
Wakuu naomba kuuliza kama kuna vidonge asilia vya kutibu tatizo kutosikia vizuri, kama tiba hiyo ipo ni wapi naweza kuipata kwa jijini Dar, na vipi gharama ya yake hadi kupona?na ni dozi ya muda gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini unaulizia vidonge vya tiba asilia?
Umeshajaribu matibabu ya hospitali ikashindikana?!
Hali hio imeanza lini?una infection kwenye masikio?
Kama ni hali umezaliwa nayo nenda kwa daktari wa masikio ukafanyiwe uchunguzi masikio yako.
Mkuu kwa tatizo hili sijaenda hospitali ila nina hakika kuwa hospital hakuna tiba zaidi ya kukushauri ununue kifaa cha kuongeza kusikia.
Usijipe uhakika. Nenda hospitali utashauriwa. Hizo tiba za jadi utaliwa tu hela zako. Mie nina mshkaji anavaa kifaa cha kusikia na yuko bomba tu, ni afisa wizara moja na ukatibu mkuu utamuangukia any minute. Usijinyanyapae bwana, nenda ukapate ushauri kwa ENT.

Kuna mtalaam mmoja yupo mjini Pemba anaweza kukusaidia kukutibia hayo matatizo ya kutosikia vizuri ngoja nitafute Contact zake nitakujuulisha inshallahWakuu naomba kuuliza kama kuna vidonge asilia vya kutibu tatizo kutosikia vizuri, kama tiba hiyo ipo ni wapi naweza kuipata kwa jijini Dar, na vipi gharama ya yake hadi kupona?na ni dozi ya muda gani?
Wakuu naomba kuuliza kama kuna vidonge asilia vya kutibu tatizo kutosikia vizuri, kama tiba hiyo ipo ni wapi naweza kuipata kwa jijini Dar, na vipi gharama ya yake hadi kupona?na ni dozi ya muda gani?
UPDATE
Niliufuata ushauri wa wanajukwaa hili kwamba niende hospital kufanya uchunguzi wa kitaalam.
Siku chache zilizopita nilionana na ENT wa hospitali binafsi, nikafanyiwa vipimo, tatizo hakuliona zaidi ya kuniambia kuwa usikivu umepungua, hivyo akashauri nitumie kifaa cha kuongeza usikivu.
ENT huyo akanimbia kuwa hakuna tiba yoyote zaidi ya kutumia hicho kifaa.
Nikapata wazo la kugeukia hizi clinic zetu za tiba asilia kama nilivyoeleza mwanzo, lakini ni vizuri kama nitapatiwa maelekezo ya herbalists wanaotoa matibabu ya tatizo hili.
Mimi Dawa ninayo nitafute nitakupa kwa gharama lakini. Unaweza kunitafuta kwa bonyeza hapa.MawasilianoCc: MziziMkavu King'asti & co.