Naweza kupata wapi ng'ombe aina ya Fleckvieh, ambayo ni the second largest dairy breed in the world?

Hawa Ng'ombe wapo vizuri sana halafu pia ni fursa mtu akiweza kuwapata na kuwauza hapa kwetu
 
hii kitu inapatikana Peramiho kwa Benedictine Fathers tulikuwa tunafuga hawa ilikuwa baalaa mtaani dume likitoka niliwajengea reserve ya majani ya gorofa mbili nawakamaliza wanakula sio mchezo ujipange na wanafumilia magonjwa sio kama freshean ambao kwenye joto hawawezi kuzalisha maziwa kwa wingi.

 
Kwa mujib wa sifa za hawa ng'ombe sio unaowazungumzia maan sifa yao hawali sana wanatoa maziwa mengi pia ni ng'ombe wanaohimili magonjwa ,mkuu huenda unzungumzia ng'ombe wanaofuga masai
 
nenda kijiji cha ifunda, iringa uliza tu kwa mzungu wa ngombe, anauza madume na mbegu(sperm anauza $3,000) pia na mara nyingi hupeleka ngombe wake huko kwenye maonyesho kenya na south africa.
Mzee sperm doller elfu tatu?? Zina ujazo gani?
 
Kuna jamaa yangu ameagiza hawa ngombe kutoka Germany hapa hapa arusha anataka kuanza biashara ya maziwa
 
Kuna jamaa yangu ameagiza hawa ngombe kutoka Germany hapa hapa arusha anataka kuanza biashara ya maziwa
Mkuu akileta tupe mrejesho na mm nahtaji, ikibd akija na waakiba tufanye biashara!
 
Wakuu mkipata info zaidi mtupe hapa angalau nikipata wawili wakuanzia siyo mbaya
 
 
Mkuu hawa ng'ombe wanapatikana tengeru, au kongwa kwenye kituo cha utafiti, ila ukitaka kuwafuga uwe vzr, wanakula sana na maji wanakunywa Lita 40 hadi 60 kwa siku. Na ukiwa na wawili au watatu uhakikishe una pa kusupply maziwa.
 
CHASHA FARMING,,,makala zako nyingi za ufugaji wa kuku zilinipa sana faida,,,,Mungu akubari mkuu Chasha
 
Ulifanikiwa mkuu? Uliwachukua wapi na bei ni kiasi gani kwa muda ulionunua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…