Naweza kuthibitisha uhalisia wa VISA niliyotumiwa?

Kichwa cha thread kinasema umetumiwa visa, post yako inasema umetumiwa form ya visa.

Mpaka hapo ushatuchanganya.
 
Sasa shule huwa mnakwenda kusomea nini? Tena mwanachuo kabisa!
 
Unapigwa mchana kweupe.
Na ubaya anayepigwa ukitaka kumwambia kuwa anapigwa anakuona wewe una wivu.
Hakunaga visa za style hiyo. Yani kama ameweza kukusaidia hayo yote ashindwe kukulipia $80
 
Naomba nitumie ushauri huu, kama ulivyo
huna haja ya kutumia huo ushaur mkuu, huyo ni tapel achana naye, visa zinatolewa kwenye balozi na form ya kuomba visa zinapatikan huko huko au kwenye websites zao, hv official language ya canada ni kifaransa?
 
huna haja ya kutumia huo ushaur mkuu, huyo ni tapel achana naye, visa zinatolewa kwenye balozi na form ya kuomba visa zinapatikan huko huko au kwenye websites zao, hv official language ya canada ni kifaransa?
Asante huy me nimemkataa, ila Kifaransa pia ni lugha official canada
 
huna haja ya kutumia huo ushaur mkuu, huyo ni tapel achana naye, visa zinatolewa kwenye balozi na form ya kuomba visa zinapatikan huko huko au kwenye websites zao, hv official language ya canada ni kifaransa?
Quebec Canada wanaongea Kifaransa kama official language.
 
Uelewa wako mdogo sana aisee! Si ujiongeze hata usome taratibu za Visa online?
Mkuu mambo ya safari na shule ni vitu tofauti kabisa wapo watu waliamini wakisoma watapata kazi Tanzania na maisha yataenda baadae wanakutana na changamoto za Ajira ndio wanakuja kujiongeza kwenye Visa inakua topic mpya kwao sass hivi graduate hana Passport waka driving licence unategemea nini na vyote hivyo vinataka hela kwa maisha yetu haya inabidi vionekane ni anasa...mwanafunzi akienda kuomba Passport maswali atakayoulizwa kesho arudi tena wakati huo huo mtoto wake wa miaka minne ashamkatia Passport...
 


Graduate anaweza thibitisha almsot everything online, huitaji kujua kuhusu visa, unaitaji ku search information kuhusu visa
 
Kimbia mm travela najua nachosema.unachat na mzungu pori
 
Ni kweli hao majamaa wa Lagos hawafai, japo nimeona nisikurupuke kwanza, niulizie uhalisia naona sasa nimpotezee tu kabla sijalizwa
Huyo Jamaa ni Mjanja sana, Quebec ndo Jimbo pekee Canada ambapo Lugha rasmi ni Kifaransa! Ulivyosema alikutumia Documents zikiwa kwa Lugha ya Kifaransa, nikasema YES...!

Miaka 3 nyuma ilikua kidogo niende Quebec, nina rafiki pale, nilishaanza kujifunza mpaka Kifaransa, coz kwa aina ya Visa ambayo nilikua nataka, ningefanyiwa Interview na Ubalozi kama angalau namudu hata kujielezea kwa Kifaransa, sema safari yenyewe ikaingia Mdudu!

Naona Spirit yako, mimi nna uzoefu na mambo ya safari, ngoja nikupe idea....!

Zipo baadhi ya Nchi ambazo Zinaweza ku issue Visa yako huko huko kwenye hiyo nchi, Canada sio Moja wapo, kwa Canada kama una mwenyeji, yeye anachoweza kusaidia ni kukutumia barua ya Invitation, ambapo anakua amejifunga kukuhudumia wewe kipindi chote ukiwa huko, hasa kwa Visiting Visa, labda kukugharamia ticket ya go and return, na vitu vingine, hiyo barua ndo unaweza ku attach na Documents zako kwenda Ubalozini wewe mwenyewe kuomba Visa!

Ukiacha mipango yako ya kuomba ufadhiri wa masomo, tafuta Marafiki wa kizungu, tokea hapo hapo Quebec, tengeneza urafiki bila kuonyesha lengo lako, urafiki ukikolea, anza kuchomekea kuhusu Dhamira yako, mwambie rafiki yako, huitaji yeye akutumie pesa wala nini, unachoomba na akutumie tu mwaliko, na kwamba kuhusu ticket ya Ndege utagharamika mwenyewe, sidhani kama ticket ya ndege itakushinda, ukiweka nia, ndani ya miezi 3 ushapata rafiki tayari....!
 
Asante sana kaka [emoji120] ninalifanyia kazi hili
 
Naomba nitumie ushauri huu, kama ulivyo
Acha kujigonga gonga wewe. Utapigwa. Huyu 100% ni tapeli. Visa inatolewa na ubalozi na inabidi uende, ujaze fomu ulipie huko ubalozini, uhojiwe na ukikubaliwa ndiyo unapewa visa. Wewe endelea kuwasiana naye tu lakini unapoteza muda wako bure na pengine aje akushawishi utume fedha...
 
Unampotezea muda wewe. Watu wengine bwana. Huyu huoni ni tapeli anataka kumtapeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…