Naweza kuwashitaki CRDB ili walipe fidia kwa usumbufu na kadhia?

Naweza kuwashitaki CRDB ili walipe fidia kwa usumbufu na kadhia?

Kabulala

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2019
Posts
695
Reaction score
936
Leo nimeenda Bank kuchukua pesa ambazo kabla sijaanza kuwapatia wanihifadhie tulipeana masharti.

Cha kushangaza Leo nimeenda branches mbili zote walinzi wao (ambao hawakuwepo wakati nawekeana makubaliano na bank kuhusu vigezo na masharti) wakanizuia kuingia ndani kuchukua pesa zangu Kwa kigezo eti sijavaa Barakoa..na Mimi nikivaa Barakoa nashindwa kupumua.

Na kutopata access ya pesa yangu niliyowapatia Kwa makubaliano maalumu (Barakoa haikua mojawapo) Leo nimepata hasara na usumbufu Mkubwa.

Naomba wanaojua Sheria za Haki za mteja wanishauri kama naweza KUWASHITAKI CRDB ili walipe fidia Kwa usumbufu na kadhia waliyonipatia bila ata taarifa ya awali..!?
 
Leo nimeenda Bank kuchukua pesa ambazo kabla sijaanza kuwapatia wanihifadhie tulipeana masharti,cha kushangaza Leo nimeenda branches mbili zote walinzi wao (ambao hawakuwepo wakati nawekeana makubaliano na bank kuhusu vigezo na masharti) wakanizuia kuingia ndani kuchukua pesa zangu Kwa kigezo eti sijavaa Barakoa..na Mimi nikivaa Barakoa nashindwa kupumua..na kutopata access ya pesa yangu niliyowqapatia Kwa makubaliano maalumu (Barakoa haikua mojawapo) Leo nimepata hasara na usumbufu Mkubwa..naomba wanaojua Sheria za Haki za mteja wanishauri kama naweza KUWASHITAKI CRDB ili walipe fidia Kwa usumbufu na kadhia waliyonipatia bila ata taarifa ya awali..!????
Tamko la kuvaa barakoa sehemu za umma limewekwa na Crdb au serikali?
 
Unaweza kufungua kesi lakini grounds zako zitakua weak dhidi ya zile za CRDB. Unaweza kupoteza gharama nyingi za kufungua kesi na iwapo CRDB watashinda utalazimika kuwalipa gharama za kesi (costs). Hivyo sikushauri kufungua kesi maana you have a very little chance of winning.
 
Kama una cheti cha daktari kuhusu afya yako unapovaa barakoa nenda mahakamani. Wagonjwa wa pumu hawashauriwa kuvaa barakoa
Too general statement.
Mimi ni mgonjwa wa pumu, ila barakoa hainiletei shida yoyote; Full time nikiwa outdoors nipo na barakoa, maana daktari aliniambia na hii pumu yangu, nikipata COVID, chances za kumrudia muumba ni kubwa kuliko za ku-survive.
 
Leo nimeenda Bank kuchukua pesa ambazo kabla sijaanza kuwapatia wanihifadhie tulipeana masharti.
Kwani crdb ndo wameleta korona Hadi useme wamekusumbua kwa ajili ya barakoa? Vaa barakoa maana Ni ugonjwa na ungekuwa na malaria usingesema crdb wanakusumbua wakati unaumwa.
 
😁😁 hii Nchi imechezewa sana....

Au nasema uongo ndugu zangu?

Akiulizwa hasara aliyoipata kwa kushindwa kutoa pesa zake anaweza kukosa ushahidi.

Watu wanafikiri pesa inatolewa tu kisa umefungua kesi.

Siku anaenda kuweka hiyo pesa hao askari si aliwaona hapo jengoni? Mbona hakuuliza wanahusikaje na makubaliano ya yeye kuweka pesa?
 
Haki Yako isi-impede haki ya Mwingine

Una uhakika kwenye vigezo na masharti ya mkataba wenu kulikuwa na clause kwamba nitaingia vyovyote vile kwenye Benki, na hili la Barakoa kwenye Benki hata wenyewe sio wanapenda ni kwamba inabidi sababu kwa wao pia ni rahisi matapeli kuwaibia sababu sura zao hazionekani kwahio ni vigumu kujua anayehudumiwa ni nani?
 
Leo nimeenda Bank kuchukua pesa ambazo kabla sijaanza kuwapatia wanihifadhie tulipeana masharti.

Cha kushangaza Leo nimeenda branches mbili zote walinzi wao (ambao hawakuwepo wakati nawekeana makubaliano na bank kuhusu vigezo na masharti) wakanizuia kuingia ndani kuchukua pesa zangu Kwa kigezo eti sijavaa Barakoa..na Mimi nikivaa Barakoa nashindwa kupumua.

Na kutopata access ya pesa yangu niliyowapatia Kwa makubaliano maalumu (Barakoa haikua mojawapo) Leo nimepata hasara na usumbufu Mkubwa.

Naomba wanaojua Sheria za Haki za mteja wanishauri kama naweza KUWASHITAKI CRDB ili walipe fidia Kwa usumbufu na kadhia waliyonipatia bila ata taarifa ya awali..!?
Utapoteza muda bure.
 
Mkuu wewe nenda tu.

Barakoa ni sehemu zenye mikusanyiko..sasa wao wathibitishe wewe ulienda kwenye mikusanyiko..

Kuna social distance ingeweza kutumika...kumbuka benki ili wakulipe wanahitaji pia utambuzi wa sura yako.

Hivyo hawana grounds za kukushinda mkuu. Wakulipe fidia tu.

Walinzi wamekaririshwa tu.
 
Kwenye sheria / mikataba kuna kitu kinaitwa FORCE MAJUERE
Nakushauri ujielimishe kuhusu hiyo dhana utaelimika Sana na utaachana na hayo mawazo yako.
Epidemic, endemics, wars, earthquakes, floods ni baadhi ya vitu vinavyoweza kufrustrate mkataba na aliyeathirika hawezi kufidiwa .
Korona ni mojawapo ,watu kibao wamepoteza ajira na vipato kwa mamilioni na hawakwenda kushtaki sehemu yeyote.
Inaonekana una njaa Sana unajifanya kuchungulia kila fursa hiyo ndugu siyo fursa,
vaa tu barakoa kachukue fedha zako au tumia simu banking au ATM machine
 
Utapoteza muda bure.
Jamaa inaonyesha ana njaa sana, hamna kitu Kama hicho .
Kama kingekuwepo mabenki Mengi yangefilisika kutokana na hili janga la korona.
Force majuere ipo kulinda patokeapo majanga kama haya
 
Too general statement.
Mimi ni mgonjwa wa pumu, ila barakoa hainiletei shida yoyote; Full time nikiwa outdoors nipo na barakoa, maana daktari aliniambia na hii pumu yangu, nikipata COVID, chances za kumrudia muumba ni kubwa kuliko za ku-survive.
Pole Sana mkuu,Allah akuvushe salama katika kipindi hiki
 
Back
Top Bottom