Naweza kuwashitaki CRDB ili walipe fidia kwa usumbufu na kadhia?

Naweza kuwashitaki CRDB ili walipe fidia kwa usumbufu na kadhia?

Leo nimeenda Bank kuchukua pesa ambazo kabla sijaanza kuwapatia wanihifadhie tulipeana masharti.

Cha kushangaza Leo nimeenda branches mbili zote walinzi wao (ambao hawakuwepo wakati nawekeana makubaliano na bank kuhusu vigezo na masharti) wakanizuia kuingia ndani kuchukua pesa zangu Kwa kigezo eti sijavaa Barakoa..na Mimi nikivaa Barakoa nashindwa kupumua.

Na kutopata access ya pesa yangu niliyowapatia Kwa makubaliano maalumu (Barakoa haikua mojawapo) Leo nimepata hasara na usumbufu Mkubwa.

Naomba wanaojua Sheria za Haki za mteja wanishauri kama naweza KUWASHITAKI CRDB ili walipe fidia Kwa usumbufu na kadhia waliyonipatia bila ata taarifa ya awali..!?
Acha ujinga wewe,kuna neno moja unatakiwa kulielewa ''Vigezo na Masharti kuzingatiwa" kaa ulitafakari ilo neno,ni sawa na utaratibu wao bank wanaposema bank kufungwa saa 10 kamili na wewe ukafika saa 10 na dakika 2 hawawezi kukufungulia mlango hata kama iyo hela unayotaka kutoa unaenda kumuuguza mgonjwa ama dharura yoyote ile hawawezi kukufungulia,huo ndio utaratibu wao so kaa kwa kutulia
 
Back
Top Bottom