Nawezaje kuacha uraibu wa kubeti (Betting)?

Biashara yangu inategemea sana instagram, lazma niwe na smartphone
 
URAIBU WA KUBETI UNAVYOWAWAMALIZA VIJANA.
Na Thadei Ole Mushi.

Kama hujawahi kushiriki mchezo wa bahati nasibu maarufu kama "KUBET" Basi utakuwa umewahi kuusikia.
Kubet kama wenyewe wanavyouita ni kitendo cha kufanya predictions ya matokeo ya mchezo fulani kabla haujachezwa.

Mchezo huo unaweza ukawa mpira wa miguu, nashindano ya magari, Riadha na kadhalika, japokuwa kwa hapa Tanzania wachezaji wengi wa Kamari hii hutabiri matokeo ya mpira wa miguu katika Ligi mbalimbali.

Kama tujuavyo Kubet ni kamari iliyohalalishwa na kamari ni Kitendo cha ku risk-Fedha au kitu cha thamani kwa kutegemea kushinda ili upate fedha zaidi. Kwa maana hiyo Kamari hii inakwenda na option mbili kubwa kupoteza au Kupata. Unachopoteza hapa ni fedha au kitu chako cha thamani ulichokitumia kuchezea kamari hiyo.

# Kwa sasa madhara ya moja kwa moja hayajaonekana juu ya mchezo huu ambao umejumuishwa kwenye michezo ya bahati nasibu nchini.

# Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vituo vya uchezeshaji wa mchezo huu... na unachezwa na rika zote kwenye jamii.

# Pamoja na kwamba vitabu vya dini vinakataza kwa pande zote kwa wenzetu Waislam na Wakristo ila vijana wake wamekuwa ndio wachezaji wakuu wa mchezo huu. Cha ajabu hata viongozi wetu wa dini wanahalalosha uchezaji wa kamari kwa kuwa wala hawakemei. Nasema wamehalalisha kwa kuwa hawakatazi na wala hawajaweka nguvu yoyote kupambana na swala hili kiimani.

MADHARA YAKE NI YAPI?
Madhara ya kubet ni mengi sana japokuwa makampuni yanayoendesha michezo hii wanajiinhizia fedha nyingi sana.
Kwa kuwa mchezo huu umekuwa ukichezwa sana na vijana ambao wengine wapo mashuleni na wengine ndio wazalishaji mali basi wamekuwa wakipoteza muda mwingi sana.

Ili uweze kuucheza mchezo huu vizuri itakulazimu kujifunza na kuelewa mambo mengi ya msingi katika mchezo husika. Mfano itakulazimu kuzielewa odds zinazotolewa za matokeo mbalimbali. Uwe up to date na takwimu zote kuhusiana na mechi husika kama vile, wachezaji majeruhi, walio katika fomu, waliosimamishwa, hali ya hewa, ubora wa wapinzani, wapi mechi zinachezwa na mambo mengi mengine ambayo yatakulazimu kushinda mitandaoni au kwenye vijiwe vya Soka ili kupata taarifa zote hizo muhimu.

Kama ni mwanafunzi huyu moja kwa moja ataathirika kitaaluma na kama ni mzalishaji mali ataathirika kiuchumi kutokana na upotevu mkubwa wa muda na uvivu.

# Athari nyingine ni kuongezeka kwa magonjwa yabPresha kwa wachezaji. Kwa sasa athari hii haijaonekana moja kwa moja ila huko tuendako hili litajitokeza.

Wachezaji wengi wa mchezo huu wamekuwa wakiishi maisha ya wasiwasi na Presha wakisubiri timu zao walizobet zishinde ili wapate fedha za chapchap. Kama mchezaji kamari hii atakuwa anafuatilia mchezo husika na timu aliytabiri kushinda haielekei kushinda basi huwa na wakati mgumu kiafya.

Pamoja na hayo mchezo huu kwa vijana unachochea ujambazi na wizi. Kama ilivyokuwa kwa vijana waliokuwa na Uraibu wabkutumia madawa ya Kulevya basi mchezo huu nao umeanza kuelekea kuwa na watu wenye uraibu.
Binafsi nimeshawahi kufuatwa na vijana zaidi ya sita wakikopa fedha za kwenda Kubet. Yaani kuliko aache bora akope what if ataikosa fedha hiyo? Basi ataanza udokozi na baadaye atakuwa mwizi kabisa.

Kwa Watu wazima wamekuwa wakitumia fedha za familia kwenye mchezo huu. Badala ya kupeleka mahitaji ya msingi nyumbani anaona ni bora atumie fedha hizo kujaribisha kama anaweza kuambulia chochote kitu.

# HUKO TUENDAKO
Tanzania ijiandae kuwa na vijana wengi walioathirika kiafya kutokana na mchezo huu.
Kwa hii kasi ya ueneaji kwa hapa nchini tuanze kufikiria kuanzisha taratibu za Rehabilitations. Kwa wenzetu wazungu wameshaanza kukumbwa na matatizo makubwa ya kubet na wameshaanzisha vituo vya kufanya rehabilitations.
# Kama hujaanza kucheza michezo hii usifikirie kucheza na viongozi wetu wa dini waseme waziwazi kuwa ni kinyume na taratibu za dini zetu.

# Serikali ione kwa jinsi gani inaweza kuwanasua vijana hawa kwenye huu uraibu na kuwaelekeza kwenye maswala ya Uzalishaji mali zaidi. Hawa kina Tarimba Abbas wanatumalizia nguvu Kazi huku wao wakineemeka.

# Na kwa sasa kila mtu anawaza kuanzisha mchezo wa bahatu nasibu nchini anajua tumeshapata uraibu wa kutosha hivyo ni rahisi kuamini tunaweza kupata fedha za chap chap.

# Wachina nao wamekuja na mashine zao za kutumbukiza mia mbili mia Mbili. Nendeni kwenye hivi vituo muone utitiri wa vijana amabo hawana kaz
 
Nilikuwa addict wa gambling asee,Nilikuwa Bingwa wa kuwaelekeza watu kila aina ya option..Nilianza bet 2010 pindi ndiyo betting inaanza shika kasi Nilipigwa 900k Casino pesa ya Ada Casino..Mikeka ndiyo usiseme aseee..

Nilikuwa chuo mwaka wa Pili back in 2014..Nikakaa nikawaza nikaona hii sio direction nayotakiwa kuwa...its been 8 years since nimebet na kuingia Casino.

Ni utayari tuu Kaka,Hakuna anayeweza kukushauri zaidi ya wewe mwenyewe na halmashauri yako ya kichwa..
 
Uchapwe viboko mia kidogo...wamekushauri uache kufatilia mpira unasema ushajaribu ikashindikana...wamekwambia ufute App na uuze smartphone unasema haiwezekani....kiukweli kuacha na kutokuacha ni juu yako na Nafsi yako iamue vipi sisi hatuna chakukushauri na ata wakija kukushauri akili yako itarudi kulekule...kwanza wakamaria tukionaga jitu linaanzisha Uzi wa Ivi unatamani ulipasue...tukutane kwenye uzi wetu pendwa wa (WAZEE WA KUWEKA MIKEKA....)

NAWASILISHA
 
Mtuache bwana
Kamari ipo enzi enzi na amna kitu kimebadilika duniani
 
Jaribu kwa kupunguza frequency ya kubeti,let say bet mara moja siku ya mechi muhimu tu,ukipata sawa ukipoteza poa,kama utaweza jiwekee kiwango flani tu ambacho utakitumia na uko tayali kukipoteza, usichukulie bet kama ni chanzo cha kipato,bet for fun,in general kuacha inahiji uamuzi binafsi na discipline ya hali ya juu sana.
 
Habari ndugu na jamaa!
Natumai mko salama, twende moja kwa moja kwenye mada...

Nimekua na uraibu sugu naweza kusema wa mchezo wa betting! Mchezo huu nimeanza toka nikiwa kidaro cha sita 2015 (shule yetu ilikua na uhuru sana wa kutumia simu)...
Kuanza ni maamizi ya dhati kutoka kwako mwenyewe mkui hakina ushauri utakaokusaidia.

Mimi niliamua siku moja tuna nikaacha.

Hasara umekwishaiona ni kuchukua uamuzi uache kubet hapa hata upewe ushauri wa dunia nzima kama hujaamua utarudi tu
 
Kinachofanya wengi kuwa waraibu ni kuwa na matarajio makubwa.

acha kudhani kuwa betting itakutoa kimaisha. utajikuta tu unapunguza kama si kuja kuacha kabisa.
 
Kukaa na sim ndogo sitaweza kwa maana fani/biashara nayofanya natumia zaidi Instagram. Ni lazma kila siku nipost
Mimi natamani tu kujua hiyo biashara yako inayo kuingizia kipato cha elfu 20 - 70 kwa siku.

Kuhusu hiyo ishu yako ya kubet, kiukweli sina namna ya kukusaidia.
 
betting na forex ushenzi mtupu kuna lishamba litakuja tetea forex wakati tunajua siri zote
 
Mabadiliko halisi huanzia kichwani. Wala husiuze simu wala husiache kufuatilia mpira,kitu muhimu amua kutoka moyoni kuwa umeacha na nakuhakikishia utaacha kweli. Hakuna dawa ya hilo ni wewe na akili yako.
 
Dahhh uraibu wa kubeti sitokuja kuusahau, Yani wakati wenzetu wanaovuta sigara wanasema tunaskia arosto we unawaona kama wanaigiza hivi

Nashkuru Mungu nilifanikiwa kuacha tangu mwaka 2017, haikuwa kazi rahisi ata kidogo, ila baada ya kufanya tathmini ya pesa nilizompa muhindi na ambazo yeye kanikopesha niliona sina future nzuri

Huu mchezo unawalemaza vijana wengi Sana kipindi ambacho wapo chuo, maana hela ni uhakika ata kama hana Mkopo anajua atapiga kizinga nyumbani na watamtumia

ila baada ya kuingia mtaani ndio arosto inakolea sasa, usipokuwa makini unaweza kuanza kupita na vihela ambavyo vinazagaa zagaa sebuleni alafu case wanapewa madogo

Kuacha kubeti ni maamuzi Tu mkuu ata haiitaji ushauri wa mtu, me niliacha baada ya kujaribu kuhesabu pesa nilizomchangia muhindi, nikakuta yeye amechukua kama 2M yangu ndani ya semester 1, alafu me kanikopesha kama 800k

Nikawaza nilipotoa hela zote hizo ni wapi mbona me sina uwezo wa kupata 2M ambayo haina kazi, nikagundua nilikuwa napata kutoka vyanzo vya mapato vya wengine maana vizinga vilikuwa vingi Sana wakati nasoma utazani mtoto wa kike

Ndipo nilipojua huu ni ugonjwa na natakiwa kuutafutia Tiba kabla haujakomaa, sema me niliacha siku nzuri maana kesho yake nikampiga muhindi 700k kupitia Mkeka nilioweka usiku kabla ya kupiga mahesabu kama prof Asadd CAG, kesho yake nikaamkia Posta kumenya PC mpyaaaaa
 

Asante sana mkuu, nimekuelewa vzr
 
Mimi natamani tu kujua hiyo biashara yako inayo kuingizia kipato cha elfu 20 - 70 kwa siku.

Kuhusu hiyo ishu yako ya kubet, kiukweli sina namna ya kukusaidia.

Ni kazi ambayo inahitaji ujitoe akili kidogo, usiwe na aibu na kujiona ww msomi, lkn kwa kiasi chake inakupa pesa ya kula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…