Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi naona kwanza ungeacha kufatilia mpira kbsa ratiba zote potezea alafu futa hizo app kwenye simu yakoHabari ndugu na jamaa!
Natumai mko salama, twende moja kwa moja kwenye mada.....
Mtuache bwanaURAIBU WA KUBETI UNAVYOWAWAMALIZA VIJANA.
Na Thadei Ole Mushi.
Kama hujawahi kushiriki mchezo wa bahati nasibu maarufu kama "KUBET" Basi utakuwa umewahi kuusikia.
Kubet kama wenyewe wanavyouita ni kitendo cha kufanya predictions ya matokeo ya mchezo fulani kabla haujachezwa.
Mchezo huo unaweza ukawa mpira wa miguu, nashindano ya magari...
Kuanza ni maamizi ya dhati kutoka kwako mwenyewe mkui hakina ushauri utakaokusaidia.Habari ndugu na jamaa!
Natumai mko salama, twende moja kwa moja kwenye mada...
Nimekua na uraibu sugu naweza kusema wa mchezo wa betting! Mchezo huu nimeanza toka nikiwa kidaro cha sita 2015 (shule yetu ilikua na uhuru sana wa kutumia simu)...
Biashara gn hiyo mkuuBiashara yangu inategemea sana instagram, lazma niwe na smartphone
Mimi natamani tu kujua hiyo biashara yako inayo kuingizia kipato cha elfu 20 - 70 kwa siku.Kukaa na sim ndogo sitaweza kwa maana fani/biashara nayofanya natumia zaidi Instagram. Ni lazma kila siku nipost
Dahhh uraibu wa kubeti sitokuja kuusahau, Yani wakati wenzetu wanaovuta sigara wanasema tunaskia arosto we unawaona kama wanaigiza hivi
Nashkuru Mungu nilifanikiwa kuacha tangu mwaka 2017, haikuwa kazi rahisi ata kidogo, ila baada ya kufanya tathmini ya pesa nilizompa muhindi na ambazo yeye kanikopesha niliona sina future nzuri
Huu mchezo unawalemaza vijana wengi Sana kipindi ambacho wapo chuo, maana hela ni uhakika ata kama hana Mkopo anajua atapiga kizinga nyumbani na watamtumia
ila baada ya kuingia mtaani ndio arosto inakolea sasa, usipokuwa makini unaweza kuanza kupita na vihela ambavyo vinazagaa zagaa sebuleni alafu case wanapewa madogo
Kuacha kubeti ni maamuzi Tu mkuu ata haiitaji ushauri wa mtu, me niliacha baada ya kujaribu kuhesabu pesa nilizomchangia muhindi, nikakuta yeye amechukua kama 2M yangu ndani ya semester 1, alafu me kanikopesha kama 800k
Nikawaza nilipotoa hela zote hizo ni wapi mbona me sina uwezo wa kupata 2M ambayo haina kazi, nikagundua nilikuwa napata kutoka vyanzo vya mapato vya wengine maana vizinga vilikuwa vingi Sana wakati nasoma utazani mtoto wa kike
Ndipo nilipojua huu ni ugonjwa na natakiwa kuutafutia Tiba kabla haujakomaa, sema me niliacha siku nzuri maana kesho yake nikampiga muhindi 700k kupitia Mkeka nilioweka usiku kabla ya kupiga mahesabu kama prof Asadd CAG, kesho yake nikaamkia Posta kumenya PC mpyaaaaa
Mimi natamani tu kujua hiyo biashara yako inayo kuingizia kipato cha elfu 20 - 70 kwa siku.
Kuhusu hiyo ishu yako ya kubet, kiukweli sina namna ya kukusaidia.