Nawezaje kubadili jina kwenye vyeti vyangu

Nawezaje kubadili jina kwenye vyeti vyangu

Joined
Aug 2, 2021
Posts
6
Reaction score
3
Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri mdogo kisha mama yangu akaolewa tena.

Kwa sasa nimemaliza kidato cha nne nataka kwenda chuo ila nahiitaj kutumia jina la baba yangu mzazi kabla sijaingia chuoni msaada jamani nifanye nini?
 
Nenda mahakamani na vyeti vyako hasa vya elimu uwaombe wakusaidie kisheria.Naamini utakuwa umesaidiwa.LAKNI:Mama yako ana taarifa na unayotaka kutafanya?
 
Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri mdogo kisha mama yangu akaolewa tena.

Kwa sasa nimemaliza kidato cha nne nataka kwenda chuo ila nahiitaj kutumia jina la baba yangu mzazi kabla sijaingia chuoni msaada jamani nifanye nini?
Andaa doc inaitwa deed poll zinakuwa tatu na passport 3
Peleka kwa msajiri wizarani ardhi isajiriwe
Hapo utakuwa umefanikiwa
Deed poll zinaandaliwa nacmwsnasheria
 
Andaa doc inaitwa deed poll zinakuwa tatu na passport 3
Peleka kwa msajiri wizarani ardhi isajiriwe
Hapo utakuwa umefanikiwa
Deed poll zinaandaliwa na mwanasheria
Hapo haitakuwa na madhara yoyote mfano kwenye suala la ajira
 
Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri mdogo kisha mama yangu akaolewa tena.

Kwa sasa nimemaliza kidato cha nne nataka kwenda chuo ila nahiitaj kutumia jina la baba yangu mzazi kabla sijaingia chuoni msaada jamani nifanye nini?
Muone wakili aliyekaribunawe atakuandalia kiapo (DEED POLL) then atakuongoza ofisi inayohusika namaswala hayo serikalini.
 
Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri mdogo kisha mama yangu akaolewa tena.

Kwa sasa nimemaliza kidato cha nne nataka kwenda chuo ila nahiitaj kutumia jina la baba yangu mzazi kabla sijaingia chuoni msaada jamani nifanye nini?
Mkuu kama watangulizi hapo walivyukuelekeza, pita kwa mwanasheria aliyekaribu na wewe atakutengenezea nyaraka ya kisheria (Deed poll) ambayo itaonyesha kuwa unatambulika kwa majina unayoyahitaji sasa na kuyakana yale ya zamani! Mara baada ya kukamilika itapaswa kusajiliwa kwa wizara ya ardhi.

Kumbuka kuwa zile nyaraka zako za zamani mfano cheti cha kidato cha nne hakitabadilika jina bali utakuwa ukiambatanisha nakala ya deed poll yako na cheti chako pale kinapohitajika, Hila nyaraka zote mpya baada ya deed poll zitakuwa na jina ulitakalo mkuu.

Nawasilisha.
 
Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri mdogo kisha mama yangu akaolewa tena.

Kwa sasa nimemaliza kidato cha nne nataka kwenda chuo ila nahiitaj kutumia jina la baba yangu mzazi kabla sijaingia chuoni msaada jamani nifanye nini?
Kimsingi, huwezi kubadili majina yaliyoko kwenye vyeti vyako. Majina hayo yatabaki kama yalivyo kwenye nyaraka hizo na katika Taasisi husika milele.

Isipokuwa, utapaswa kuapa na/au kuandaa Deed Poll (kama walivyoeleza waliotangulia) kwa ajili ya kusaidia kufafanua kwamba kuanzia tarehe ya Kiapo chako/usajili ya Deed Poll yako, ulianza kutumia jina jingine.
 
Njia nyingine ya asili ukiona hao wanasheria wanakuchelelesha ni hii Mkuu wangu,

Zunguruka Mbuyu wowote mara saba,litaje jina unalolitaka mara saba,yaani mfano NAAPA KWAMBA JINA LANGU LIWE ........ BADALA YA .......(Lilel lililo kwenye Cheti ambalo hulitaki) MARA SABA HUKU ukiuzunguka huo mbuyu, huku ukiwa umefumba macho na ukiwa uchi wa mnyama usiku wa manane, huku ukiwa umeshikilia vyeti vyenye jina unalotaka libadilike. Ukishamaliza nenda kwenye mwanga, tupia macho yako kwenye hivyo vyeti utaona majina yako yote yamebadilika na yatakuwa kama ulivyoomba kwenye Mbuyu.

Basi unaendelea na shughuli zako kama kawaida Mkuu wangu.

Usisahau kuleta mrejesho ukishafanya hiyo shughuli Mkuu.
 
Back
Top Bottom