Nawezaje kudhibiti matumizi ya internet Kwenye laptop yangu?

Nawezaje kudhibiti matumizi ya internet Kwenye laptop yangu?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari Wakuu. Nina laptop aina ya Toshiba ila tatizo niiiunga na WiFi hotspot ya Simu yangu ya Tecno inakula data so mchezo. Juzi tu niliiunga ili kuperuzi website kadhaa lakini ndani ya dakika tano ikawa imetafuna MB 300! Naomba msaada nifanyeje kudhibiti hii hali.
 
Weka metered connection,

Kama ni windows10 nenda kwenye settings->network&internet->Wi-Fi->[chagua jina la hotspot]->set as metered connection iweke on
Apo itazuia updates na background use nyingine
 
Nilishawahi lizwa 1Gb kwa less than 15 minutes na nliingia LinkedIn tu, window 10 usiposet vzr n jini
 
Jaribu kuangalia hizi icons hapa chini, moja baada ya nyingine kuangalia kama zipo ON au OFF

ON-OFF.png


Chukua mfano Weather App, hiyo muda wote inaji-update! Sasa kama ipo ON, lazima itakuwa inakula bundle! Mimi mwenyewe hapo juu ina maana nilikuwa natoa sadaka ya bundle.

So, click START kisha RIGHT CLICK kila app zitakazotokea upande wa kulia. Ukisha-right click, kama app husika itakupa option ya MORE, na hapo uki-click, utapata option ya ON or OFF... kwahiyo unatakiwa ku-turn OFF.
 
Back
Top Bottom