Nawezaje kuhamisha pesa toka master card kwenda paypal?

Full charge

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
1,678
Reaction score
1,617
Shikamoni wakuu, ila wadogo malhaba.
Nataka kununua saa ebay ila naambiwa eti nibadili njia ya malipo, natumia m-pesa master card nimekuwa nikiitumia kununulia vitu. Ilikuwa imeisha muda wake ila sasa nimei-update imekaa sawa ila inakataa kununua chochote, msaada jamani nimechemka.
 
Kwanza kajisajili paypal na hakikisha taarifa zako zinafanana naza kwenye master card yako na pia zifanane na zile za ebay, amazon au aliexpress baada ya hapo utasubiri paypal wakutumie ujumbe kuwa uko approved.
Then fanya miamala kwa kuchagua lipa kwa paypal.
KUMBUKA PAYPAL HATUNZI HELA ILA YEYE YUKO KATIKATI KUHAKIKISHA KUNA USAWA
 
Hii issue Vodacom hawajaiboresha. Kadi yao inadumu kwa mwezi mzima nqdhani. Ikiisha muda wake ukarenew account hauwezi kufanya tena malipo, linabaki jina tu. Nina line mbili zote nimejiunga na mpesa MasterCard ila zilishagoma kufanya malipo ninazo kama pambo tu. Wakati nafungua kwamara ya kwanza zilifanya kazi vzri tu ila baada ya kuisha muda wake na kuzisasisha , mpaka leo ni karibu mwaka sipati huduma PayPal, ukilipia unaambiwa blabla nyingi. Ubaya customer care wao wanajiona wameyapatia maisha, kiasi kwamba ukipiga unaambiwa tembelea duka la Vodacom 😠😠 fikiria uko km za kutosha toka walipo, ulipe usafiri kwenda kurekebishiwa line tu na pengine ukifika wanakupiga kiswahili. Kama una account crdb nenda activate online payment tu mkuu, voda wazinguaji tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…