Ngoja na mimi nijaribu kukujibu kutokana na uzoefu wangu huu mdogo.
Language nyingi za programming zinafanana misingi yake mfano kwa uzoefu wangu utaona language nyingi lazma zitakuwa na
- variable(initialization and declaration)
- Control Statement (if,switch)
- Iteration( while/do while/for loop) nk
- Data structure kwa OOP
- nk
Kwa upande wangu nafikiri language ya C ni nzuri sana kwa beginer kujifunza kwa sababu inakupa misingi ya programming, tofauti na language kama python na php.
Mfano kwenye variable declation upande wa C language huwa hiv int a; tofauti na kabsa na inavyofanyika kwenye python au php. Sasa mara nyingi madeveloper walitokea kwenye python au php na languages nyingine(nafikiri Ruby kama sikosei) zinazofanana na hizo hupata shida kushift kwenda lugha nyingine.
Ni rahisi sana kushift kutoka kwenye C kwenda kwenye langauge yoyote ile kwa sababu language nyingi ni C-typed
Note: Simaanishi pyhon au php ni mbaya, La hasha ni nzuri tu, na zinafanya vzr tu ila sishauri kutumika kwa beginer.
Mwl wangu mmoja aliwahi kuniambai kuifahamu langauge moja vzr inakupa asilimia 60 ya kujifunza langauge nyingine yeyote. Hivyo kama utakuwa umeijua vzr C inaweza kukupa asilimia 60 za kujifunza php, python, java na nyingine nyingi.
Kwa beginer ni vizr sana kuanza na vitabu, lkn sio mbaya pia ukitumia tutorials pamoja na reference kutoka sites husika.Hii itakusadia sana,
Usjichoshe kutaka kujua kila kitu kuhusu langauge husika.
Pia unaweza anza na tutorials video then ukaja kwnye vitabu, ila ukitaka kuanza kwenye tutorials vdeos ni vzr sana ukanunua tutorials kutoka site zinazouza course hizo mfano ( udemy.com/lynda.com) tofauti na youtube. Faida ya kununua kupitia sites hizo ni kuwa unaweza pata maoni kutoka kwa walionunu course hizo. Lkn pia inakupa faida ya kupata usadizi pale unapokwama kupitia account yako kwenda kwa instructor husika wa course. Mara nyingi course hizi hupungua hadi dola 10 za kimarekani ambapo zisdhani kama inazidi Tsh 3,5000 za kitanzania. Tsh 35,000 ni nyingi ila naamini kabsa hutajutia ukichagua course nzuri.
Baada ya kujifunza C hamia language yoyote unayotaka, kulingana na mahitaji yako, yaana kama unataka kwa developer wa web au desktop au mobibel app. Kama mdau mmoja hapo juu alivyoshauri ni vzr ujifunze kwa kufanya projects.
Ila nashauri unapoenda kujifunza langauge nyingie tofauti na C hakikisha unajifunza na framework yake ili upate urahisi wa kufanya project. Hakikisha unajua langauge husika vzr sio lazma iwe deep sana then hamia kwenye framework yake Mfano; Pyhon kuna Django framework, PHP kuna CodeIgniter, Laravel Framework, na nyingine nyingi tu, Ruby kuna Ruby On Rails framework nk
Unapoenda kujifunza langauge yoyote ni vzr ukasoma kwanza historia ya langauge husika ambapo itakueleza purpose ya hio language lkn pia itakusadia kukupa pengine hamu ya kujifunza language hio. Kumbuka kila langauge ina umuhimu wake kulingana na matumizi husika. Sidhani kama kuna langauge ni nzuri kushinda nyingine.
Hakikisha unajifunza language chache na kuzielewa vzr, hii itakufanya kuwa na muda mwingi kuzitumia langauge hizo. Pia fanya project nyingi uwezavyo zitakusadia kujua nini unatakiwa kujifunza kwenye langauge husika.
Nihitimishe sasa, usikate tamaa wakati unaposhindwa kuendelea kutokana na bugs wakati wa development hii hutokea sana, kwa asilimia kubwa matatizo mengi utakayoyapa yanaweza kuwa mapya kwako lakn sio kwa wengine. Zipo zita nyingi anazoweza pata majibu mfano stackoverflow.com
Mengine wadau wamewasilisha juu hapo.
Kila la kheri.