Nawezaje kujikinga na TB?

Mwanaoshimba

Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
61
Reaction score
82
Nimekaa kwenye gari na mtu ambaye nahisi ana TB na hajaanza kutumia dozi. Anakohoa kikohozi kikavu sana na kwa muda mrefu.

Huko nyuma alishawahi kuugua TB na kupona. Kikohozi nilichokiona leo nahisi imerudi tena, maana kikohozi kile si cha kawaida.

Sasa nauliza kwa wenye ujuzi, kuna namna ya kujikinga? Maana pia hapa nyumbani nina mtoto mchanga, imenitia hofu sana.
 
Mkuu kwani mtu anaweza kuugua TB zaidi ya mara moja???Afu kwanini usishuke kwenye gari lakini??!!!
 
Akishapona- yaani baada ya kumaliza dozi yake iwe ya vidonge au sindano basi TB hairudii tena.Zile dawa huwa zinatengeneza Kinga Fulani ndiomana mgonjwa wa TB Akishapona maranyingi kuumwa homa kama Malaria inakuwa nadra sana
 
Mkuu kwani mtu anaweza kuugua tiba zaidi ya mara moja???Afu kwanini usishuke kwenye gari lakini??!!!
Inawezekana mtu kuugua TB zaidi ya mara moja,maana hadi useme mgonjwa kapona TB inatakiwa apimwe tena makohozi kipindi anatumia dawa tena wanapimwa mara tatu na majibu yake yawe negative...wengiwao ambao wanaumwa zaidi ya mara moja ni wale waliomaliza dawa ila hawakupona
 
mara umekaa nae kwenye gari,mara nyumbani kuna kichanga? sielewi huo uhusiano.au ni wewe sema mkuu usiogope
 
Pamoja sana mkuu,asante
 
mara umekaa nae kwenye gari,mara nyumbani kuna kichanga? sielewi huo uhusiano.au ni wewe sema mkuu usiogope
Mkuu ni hivi, labda nifafanue zaidi, leo mimi nimetoka kuelekea hospital kumchukua mke wangu ambaye amejifungua. Sasa wakati nakwenda nikampa lift huyo mtu ambaye ni jirani yangu na nafahamu alishawahi kupata TB. Ndio akawa anakohoa sana, nikapata wasiwasi. Sasa kusema nina kichanga mantiki yake ni kuwa kama mimi naweza kuwa nimebeba hao bacteria itakuwaje hiki kichanga changu? Siwezi kukiambukiza?
 
Mkuu TB huwa inaambukiza kirahisi sana hasa kwa mtu ambaye hajaanza kutumia dawa. Ila kama kinga yako ya mwili ipo juu inakuwa sio rahisi kupata maambukizi. Ila kwa watoto wadogo huwa wanapewa kinga dhidi ya huo ugonjwa kwa sababu miili yao ni vigumu sana kupambana na maradhi.

Kuhusu kujirudia ni TB ni kwa mtu ambaye huenda hakutumia dozi yake vile inavyostahiki ndio maana injirudia tena na huenda pia baada ya kumaliza dozi kama alikuwa mtumiaji wa vileo vya kuchangia akawa amerudia tena kwenye mfumo ule ule wa maisha.

Hivyo basi kama ikitokea TB imekurudia vituo vya afya huwa wanampa mgonjwa dawa pamoja na sindano kwa muda wa miezi nane mfululizo tena anatakiwa ahudhurie hospital kila siku.

Ila njia nzuri ni kumshauri huyo muhusika akikohoa afunikie mdomo wake kwa kitambaa ili asiruhusu maambukizi yaenee kwa watu waliokaribu naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…