Nawezaje kujua yai limeharibika?

Nawezaje kujua yai limeharibika?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Unakuta unavunja yai na kile kiini cha njano kinasambaa na kuchanganyikana na ute hata kabla hujalikoroga. Hili yai bado zima?.

Nawezaje kujua yai limeharibika au la?
 
He! Hakuna mwenye maarifa hayo humu?
 
Kama kujua yai zima na bovu yaweke kwenye sufuria yenye maji.

Yai zima litazama na bovu litaelea.
Yapo yanayozama lakini ukilivunja unakuta kiini kinasambaa kabla hujakoroga
 
Kama kiini ni cha njano sio bovu ila kama kiini kina mchanganyiko wa damu ndio bovu. Hapo juu umeambiwa yai zima litazama,liangalie kwa makini uzamaji wake je limezama kwenye chombo cha maji au linaelea kwa chini chini. Linaloelea elea kwa chini vunjia kwenye chombo kingine maana linaweza kuwa limeanza haribika au ni zima.
 
Nimewasoma wakuu. Bila shaka nimepata somo
 
Unakuta unavunja yai na kile kiini cha njano kinasambaa na kuchanganyikana na ute hata kabla hujalikoroga. Hili yai bado zima?.

Nawezaje kujua yai limeharibika au la?
Kama ni la kienyeji, weka maji kwenye chombo halafu weka yai lako. Likielea, yaani kuonekana jepesi basi limeharibika au kuku alianza kuatamia halifai
 
Back
Top Bottom