Nawezaje kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta? Ikiwa mimi natumia gari?

Leo tena Tanzania imeshuhudia kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, dizeli na kerozini. Haya ni maumizi kwa wananchi na serikali haina namna ya kufanya kuleta aueni kwa wananchi. Bei ya mafuta kote duniani haijatulia kutokana na vita vinavyoendelea Ukraine.

Swali la kujiuliza ikiwa mishe zako zinategemea mafuta hayo NI: NAWEZAJE KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA?

Zipo njia tofauti tofauti mwananchi anaweza kuzitumia kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta ili kuweka uchumi wako stable na kuweza kuendelea na maisha mengine.

Zifuatazo ni baadhi ya njia:
1). Epuka mida ya foleni kali za barabarani
Kwa wakazi wa dar es salaam, kuna mida ambayo foleni ni shida sana. Yaani utakaa hadi ukome.
Kwa mtu anayetaka kupunguza matumizi ya mafuta kwa wanaotumia magari, ni vyema akaepuka foleni.

2) Tumia njia fupi (shortcut) kufika kwenye mishe zako.

3). Punguza mizunguko isiyokuwa ya lazima. Wengine hata kwenda saluni ambayo ipo ndani ya walking distance yeye anawasha gari.

4). Zima gari ukiona utakaa mahali kwa zaidi ya dakika 20.

5). Paki gari na anza kutumia public transport. Hii ya tano ni ikiwa umeona budget ya mafuta inaweza kuathiri ratiba za chakula, ada na matibabu.

6). Omba sana kwa ajili ya viongozi wakumbuke kuwa watanzania bado ni maskini. Hivyo ongezeko la bei ya mafuta ina athari kubwa kila nyanja.

Asanteni
Hakikisha gari Yako unafanyiwa service sahihi na Kwa wakati sahihi, pili, epuka kufunga vitu ambavyo sio recommended Kwa hio gari, ukiongeza mbwembwe kwenye gari Kuna uwezekano wa consumption kuongezeka pia (sizungumzii radio au honi)
 
Leo tena Tanzania imeshuhudia kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, dizeli na kerozini. Haya ni maumizi kwa wananchi na serikali haina namna ya kufanya kuleta aueni kwa wananchi. Bei ya mafuta kote duniani haijatulia kutokana na vita vinavyoendelea Ukraine.

Swali la kujiuliza ikiwa mishe zako zinategemea mafuta hayo NI: NAWEZAJE KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA?

Zipo njia tofauti tofauti mwananchi anaweza kuzitumia kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta ili kuweka uchumi wako stable na kuweza kuendelea na maisha mengine.

Zifuatazo ni baadhi ya njia:
1). Epuka mida ya foleni kali za barabarani
Kwa wakazi wa dar es salaam, kuna mida ambayo foleni ni shida sana. Yaani utakaa hadi ukome.
Kwa mtu anayetaka kupunguza matumizi ya mafuta kwa wanaotumia magari, ni vyema akaepuka foleni.

2) Tumia njia fupi (shortcut) kufika kwenye mishe zako.

3). Punguza mizunguko isiyokuwa ya lazima. Wengine hata kwenda saluni ambayo ipo ndani ya walking distance yeye anawasha gari.

4). Zima gari ukiona utakaa mahali kwa zaidi ya dakika 20.

5). Paki gari na anza kutumia public transport. Hii ya tano ni ikiwa umeona budget ya mafuta inaweza kuathiri ratiba za chakula, ada na matibabu.

6). Omba sana kwa ajili ya viongozi wakumbuke kuwa watanzania bado ni maskini. Hivyo ongezeko la bei ya mafuta ina athari kubwa kila nyanja.

Asanteni
Namba tano hapo 🤣🤣🙌
Hapa ni kudeal na elimination of CCM period. All these years since We got our independence nothing We can be proud of comparing to others.
 
Kwani lazima kutumia gari. Hebu tafuta ka tvs alafu tia full tank ni lita 10 sio hela kubwa ila utazunguka mpka uchoke
Ngoja tukomae na magari tu. Tutakua tunayatumia panapokua na uhitaji. Pikipiki zina changamoto nyingi maana kipindi cha kiangazi unaoga vumbi tu njiani, ikifika masika ni kunyeshewa yani hakuna afadhali...
 
Leo tena Tanzania imeshuhudia kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, dizeli na kerozini. Haya ni maumizi kwa wananchi na serikali haina namna ya kufanya kuleta aueni kwa wananchi. Bei ya mafuta kote duniani haijatulia kutokana na vita vinavyoendelea Ukraine.

Swali la kujiuliza ikiwa mishe zako zinategemea mafuta hayo NI: NAWEZAJE KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA?

Zipo njia tofauti tofauti mwananchi anaweza kuzitumia kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta ili kuweka uchumi wako stable na kuweza kuendelea na maisha mengine.

Zifuatazo ni baadhi ya njia:
1). Epuka mida ya foleni kali za barabarani
Kwa wakazi wa dar es salaam, kuna mida ambayo foleni ni shida sana. Yaani utakaa hadi ukome.
Kwa mtu anayetaka kupunguza matumizi ya mafuta kwa wanaotumia magari, ni vyema akaepuka foleni.

2) Tumia njia fupi (shortcut) kufika kwenye mishe zako.

3). Punguza mizunguko isiyokuwa ya lazima. Wengine hata kwenda saluni ambayo ipo ndani ya walking distance yeye anawasha gari.

4). Zima gari ukiona utakaa mahali kwa zaidi ya dakika 20.

5). Paki gari na anza kutumia public transport. Hii ya tano ni ikiwa umeona budget ya mafuta inaweza kuathiri ratiba za chakula, ada na matibabu.

6). Omba sana kwa ajili ya viongozi wakumbuke kuwa watanzania bado ni maskini. Hivyo ongezeko la bei ya mafuta ina athari kubwa kila nyanja.

Asanteni
Eti niombe kwa ajili ya viongozi...... Hawa hawa?
 
Yaani up nanua kluger alfu unatia wese la elf 20 kudadeki mtakomaa weka full tank acha ubabahifu kaka gari unanunua milion. 17 alfu unalia pesa za mafuta week full tank Mara mbili kwa mwezi uone kama utalialia mafuat
 
Na watu wengi wakipaki magari wakitumia usafiri wa umma +kutumia miguu ,huko juu wakuona mafuta hayanunuliki sana wenyewe bei watakuja kuweka sawa,ila watu wenye magari wakiishia kulalamika huku wanayatumia wataendelea kuburuzwa tu

Ova
Serious bro.. tunafanyiwa uhuni sana.
 
Kuandamana ndio njia pekee kuiilazimisha serikali kupunguza kodi kandamizi kwenye bei za mafuta. Kudai Katiba amabyo itaweka ukomo wa kodi inayoweza kudaiwa kwa raia. Na kuwajibisha serikali kuwa na matumizi mazuri ya kodi ili kodi ifanye yale ya muhimu kwa raia na sio matumizi mabovu ambayo yanatuumizi sisi walipa kodi kwa kudaiwa kodi zaidi.
 
Tatizo la wa Tz wengi ni kutumia umiliki wa gari kama 'status symbol'. Mtu ananunua gari ili tu aonekane ana gari kutokuzingatia uhalisia wa uwezo wake wa kipato kuweza kumiliki gari au uhitaji hasa wa hilo gari.

Unakuta mtu kapanga vyumba 2, nyumba haina parking inabidi kwenda kuipaki CCM ambapo analipia kila usiku mmoja, yote hii ni ili aonekane anamiliki gari ambayo kiuhalisia hana uwezo wala uhalisia wa kuimiliki.
Kuna watu wana magari ambayo huendeshwa siku 2 za mwanzo baada ya kupokea mshahara, siku 28 inapaki uwani, mtu anagombania bomba za DCM.

Unakuta mtu ana vitz tu lakini kucha kutwa analalamika kuhusu bei za spare na mafuta kuwa ghali.

Mtu anafanya kazi posta na anaishi Tabata au Ilala halafu anaenda kununua gari tena kwa mkopo.
Hayo maeneo kuna usafiri wa halaiki almost masaa 24.

Wengi wetu uwezo wetu ni wa boxer lakini tunakimbilia magari kupelekea kulalamika kutwa kucha kuhusu mafuta.

Ifikie wakati tuhalalishe matumizi ya Bajaj kuwa zaidi ya usafiri wa kibiashara na zitumike na watu binafsi kwa matumizi yao kama wanavyomiliki IST na Passo.

Kuigiza kuwa tajiri ni ghali kuliko kuwa tajiri.

Mkuu umenena vyema. Kuna mtu niliwahi kumshauri, alikuwa na gari ya cc ndogo akaiuza akanunua gari kubwa yaani akiwa barabarani hana tofauti na mbunge au kiongozi flani mkubwa wa serikali. Nikamwambia utakuja kuteseka mbeleni, akaona kama namwonea wivu. Ukizingatia mshahara wake ni wa kawaida sana plus makato ya mikopo benk na nature ya kazi yake hana safari za kumpa per diem (kwa mwaka mzima kipato kutokana na safari za kikazi hakizidi 3 au 4 m). Sasa hivi muda mwingi amepaki gari anawasha tu akiwa kazini zile movements za kutoka gheto alikopanga kwenda ofcn na kurudi. Nje ya hapo hawezi kwenda nayo ruti ndefu hata km 100 haendi analia mafuta.
 
Kuandamana ndio njia pekee kuiilazimisha serikali kupunguza kodi kandamizi kwenye bei za mafuta. Kudai Katiba amabyo itaweka ukomo wa kodi inayoweza kudaiwa kwa raia. Na kuwajibisha serikali kuwa na matumizi mazuri ya kodi ili kodi ifanye yale ya muhimu kwa raia na sio matumizi mabovu ambayo yanatuumizi sisi walipa kodi kwa kudaiwa kodi zaidi.
Dawa ni kupaki tu magari

Wayatumie wenyewe hayo mafuta

Watu wakomae tu na usafiri wa umma,mguu

Ova
 
Upo mji gani ndugu?Kama upo Dar na viunga vya karibu,upobadala mwingine japo una gharama za kuanzia.Iwapo gari yako inatumia petroli unaweza kufunga mfumo wa CNG(compressed natural gas).Inaweza kujipunguzia gharama kwa hadi60% Japo ipo Karaha kidogo ya kukosekana utashi wa kuruhusu vituo nchi nzima vya gasi asilia (CNG),nafikiri upo mgongano wa kimaslahi tu, biashara ya mafuta/wewe inawalipa hata watoa maamuzi nikiamini wengi wamewekezamo,hutaamini kama Dar vipo vituo viwili vinavyofanya kazi,cha ubungo na tazama tu.Cha tatu naambiwa kinajengwa mwandege na Dangote,na bado kukamilika,pia sijafahamu kama ni kwa ajili ya malori yake ama Kita hudumia pia raia.

Pia kituo kingine kina tegemewa kujengwa chuo kikuu cha UD ,nina mategemeo makubwa hizi bei za mafuta kuendelea kupanda ita saidia ku push kujenga vituo vipya vya CNG.Pia nina matumaini katibu mkuu nishati na naibu waziri mkuu wana enda kuongeza idadi ya vituo vya CNG huu ni wakati wa Naibu waziri Mkuu kutumia power yake ya Madaraka kuhakikisha vituo vya CNG vina ongezeka na kuondoa Misululu mirefu pale vetenary na ubungo kwa watu wana tumia hadi masaa matatu kwenye foleni ya kujaza gasi.Kwa nchi yetu ni aibu sasa kuwa na vituo viwili tu vya gasi kwa huduma zs public nchi nzima.
 
Back
Top Bottom