Duh pole sana mkuu, kinachosumbua watu wengi Ni kutojua njia sahihi za kupiga mswaki, kuanzia upande wa nje wa meno, ndani , juu na chini na mwisho ulimi.
Haya hata Mimi na ualimu wangu nilikuwa sijui, Ila mpenzi wangu ambaye nilikuwa nadate naye nadhani ilikuwa tumeshakutana Mara tatu tu, huenda alihisi harufu mbaya kinywani mwangu, akaanza kunieleza kuwa yeye aliumwa jino na alipoenda kwa daktari alifundishwa namna nzuri ya kupiga mswaki,(Kama nilivyo eleza hapo juu) na Mimi kwakuwa Ni mtu mzima nilihisi kuwa huyu mtu ananiambia Mimi nilianzia kuzingatia .
Nadhani tatizo liliisha maana Hadi Sasa haijawahi nambia maswala Kama hayo juu ya kinywa changu.
So Kama kweli unampenda mwambie katika namna ambayo hutamuumiza kihisia, Mimi niliambiwa kumafumbo sana