Nawezaje kumwambia mpenzi wangu kuwa ananuka mdomo?

Mnunulie Sensodyne na mswaki wa colgate kama zawadi. Mwambie atumie hio itamsaidia meno yake yawe ang'avu sana.

Akiiťumia kikamilifu huenda tatizo likaisha.
Tena akipata Sensodyne Gel itakuwa vizuri zaidi....Pia kuna hii dawa inaitwa RASYAN Ipo vizuri sana hata unavyoitumia unahisi kweli unatumia dawa na mabadiliko unayaona baada ya wiki tu kwa kupiga mswaki kihusahihi.
 

Attachments

  • IMG_20220818_121616~2.jpg
    65.9 KB · Views: 11
Utani mzuri wenye ukweli ndani yake,usimwambie direct

tumia njia nzuri itayomfanya aone kawaida harufu yake "usimshtue"

ukimshtua kama unampa taarifa za harusi atapoteza confidence 'hata mbele yako'

akili inahitajika ili kufikisha ujumbe ktk njia nzuri,wakati mwingine unaweza hata

usimwambie "kama unaishi nae" na ukamtibu tatizo lake bila yeye kujua kama unamtibu.

Akili tu inahitajika eneo hilo,usikurupuke yawezekana hata wewe una harufu zako anawaza atakwambiaje,hivyo hekima iliyoambatana na mahaba ndani yake itumike eneo hilo.
 
Usimwambie direct unachohitaji kufanya kama tatizo ni la kawaida fanya hivi

Mnunulie zawadi miongoni mwa hizo zawadi weka mswaki, dawa ya meno na mouthwash mpelekee

Siku hiyo piga nae mswaki kwa usahihi kabisa usisahau kupitisha mswaki kwenye ulimi wengi wanaogopa kutapika lakini ulimi ni muhimu tumia dk 4-7 mkimaliza ile dawa ya mouthwash wekeni kwenye kale kamfuniko kadili utakavyoelekezwa ulikonunua mjisukutue harafu nyenyueni vichwa vyenu juu sikilizia kwa sekunde kadhaa then tema,

Fanyeni hivo asubuhi na jioni wakati mmemaliza kula hata kama haupo wewe msisitize afanye hivo (tumia akili kumsisitiza sio ukurupuke atajihisi mnyonge na kupoteza kujiamini)

Kama uwezo wa matunda upo mwambie ajitahidi kula matunda hasa machungwa.

Anywe maji ya kutosha sisitiza maji ya kutosha.

Kmb, Tatizo likiendelea muone daktari.
 
Ma slay queen ndo walivyo hvyo kama hatanuka kwapa atanuka mdomo au atakupa gono yaani wanajali muonekano wa nje kuliko wa ndani.
 
Tena akipata Sensodyne Gel itakuwa vizuri zaidi....Pia kuna hii dawa inaitwa RASYAN Ipo vizuri sana hata unavyoitumia unahisi kweli unatumia dawa na mabadiliko unayaona baada ya wiki tu kwa kupiga mswaki kihusahihi.
Bei gani hii rafiki??
 
Duh pole sana mkuu, kinachosumbua watu wengi Ni kutojua njia sahihi za kupiga mswaki, kuanzia upande wa nje wa meno, ndani , juu na chini na mwisho ulimi.

Haya hata Mimi na ualimu wangu nilikuwa sijui, Ila mpenzi wangu ambaye nilikuwa nadate naye nadhani ilikuwa tumeshakutana Mara tatu tu, huenda alihisi harufu mbaya kinywani mwangu, akaanza kunieleza kuwa yeye aliumwa jino na alipoenda kwa daktari alifundishwa namna nzuri ya kupiga mswaki,(Kama nilivyo eleza hapo juu) na Mimi kwakuwa Ni mtu mzima nilihisi kuwa huyu mtu ananiambia Mimi nilianzia kuzingatia .

Nadhani tatizo liliisha maana Hadi Sasa haijawahi nambia maswala Kama hayo juu ya kinywa changu.

So Kama kweli unampenda mwambie katika namna ambayo hutamuumiza kihisia, Mimi niliambiwa kumafumbo sana
 
Ishu kama tonsil stones zinawatesa sana uwe unampeleka kwa daktari achekiwe sio kumpeleka saloon tu...Jaribu kumwambia atumie dawa nzuri kama sensodyne na kutumia mouth washa kusukutua haizidi 1500
Mkuu yeye kasema ataanza je kumwambia
 
Mwambie ukweli,
Kama uliweza kumtongoza,unashindwaje kumwambia kua ana tatizo la harufu ya mdomo?
Baada ya kumwambia mwambie unaweza kumsaidia kulitatua.
 
Mpe suprise na madawa ya meno mara kwa mara, ikibidi mteme mbona wapo wengi tu wanaonukia
Aseeeee....umemaliza vibaya. Anaweza mtema then mbeleni akamtafuta tena. Na utakuta alishampata jamaa mwingine wakapambana na tatizo likaisha.

Kuna wanaonuka tabiaa,uchafu, kiburi, uvivu uliopitiliza

Wanaonuka tamaa

Wanaonuka umalaya wa siri,

Wanaonuka visirani

Wanaonuka ulevi....

Aendelee kutafuta solution...Mdada atapona.
 
Mbinu imekaa kiukatili wa mchongo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…