Nawezaje kumwambia mpenzi wangu kuwa ananuka mdomo?

Oa kwanza ndio mdomo wake ndio utaanza kunukia.
Unanyandua tu bila wazee wake kula mahari unadhani mahusiano yenu yatakuwa na furaha na baraka.
Akiendelea kunuka mdomo niletee nimkague kwa kina.
 
Sijajua hivi inawezekanaje mpenz wako halafu unafikiria kumwambia unaanzaje. hizo ndo shida mnakuwa kwenye mahusiano bila urafiki. Unakaa naye unamwambia, trust me utakuheshimu sana ni wanaume wachache sana wanauwezo wa kuwaambia wanawake kuhusu kuwa safi.
 
Mnunulie mouthwash za kusukutua, med oral ni nzuri,tho zipo nyingi sana, mununulie na colgate maxfesh ile nyekundu nzuri sana. Wewe mpe kama zawadi.

Ila una moyo mm siwezi,hata kukubali kulala nae, kuna mwanaume alinipendaga tangu 2010 mpaka leo ila sijawahi ruhusu hata anishike mkono.

Ni ngumu kumwambia mtu ananuka mdogo. Ukona unashindwa mwache, harufu ya mdomo sio ya kuvumilia. Na watu wa hivi hawajijuagi kuwa wananuka midomo.

Matumizi kila akimaliza kupiga mswaki asukutuwe kwa dk 15. Pia kabla ya kulala apige msqaki na kusukutua.

Akifanya hayo yote ikashindikana huyo ana jino bovu akalitowe.
 
Hapo lazima hamu zitamuisha asee
 
Naomba ufanyeutafiti wa matumizi ya kitunguu swaumu kunasehemu nilisoma kuwa kinasaidia nadhani kwakumeza punje atamoja nakutafunapia...em jaribu kufatilia utanishukuru japo kwakusema asantee tu sawa
 
Hahahaha ana mpenzi mwingine wa kiume sio?
 
Ndio nini? na unatibuje?
Kuna kama vitezi flani vinaota kwenye tonsils.
vinatolewa kwa madokta wa kinywa. kila baada ya muda wa miezi kadhaa.
Kujua kama unavyo koo huwa linawasha muda flani.
 
Mtafutie dawa usimuambie onana na wataalam wa afya watakupa dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…