Nawezaje kuondoa kitambi bila kukonda?

Jaribu mkuu kujipa stress kwa mkeo halafu utuletee mrejesho mkuu!
 
Kitambi na mitako mikibwa ni mifuta iliyoshikamana sasa fanya mazoez ya hasa joging kunywa maji mengi punguza wanga na sukar
 
Bongo hata wazungu,wahindi na sasa wachina wanakuja wembamba wananenepeana kama nguruwe.

Richard S Mabala alikuja bongo mwembamba tu.
Upatatikanaji wa chakula kwa urahisi ndio Maana watu wenye vipato vya Kati ndio wenye vitambi

Huko Ulaya hela ya kula mpaka upate kitambi utaitoa wap? Mtu ameajiriwa kitu Peke anachomudu ni Chakula na pango Tu tena kwa mbinde.

Vijana na wazee Ulaya wanaweza kununua iPhone Tu na pesa kidogo za kusavs kwa ajili ya vacation kupunguza stress.

Scandinavia countries watu wanakula kwa manati Sana, Japan mtu akiona masosi kama ameona Mungu, Wana maisha magumu Sana, issue ya bajeti iko very tight hakuna kula unavyotaka
 
Yaa stress ndio kiboko
 
Nilipitia stress za kiuchumi, kudaiwa na Benki

Mbona nilipungua zaidi ya kilo 17

Hizo stress za mke, hadi baadhi ya Wanaume wenzetu wanajiua kabisa yaani 🙌
Ila mkuu kuna miili mingine ni sugu kabisa hata adaiwe kiasi gani husikii akikonda! Huwa nashangaa kabisa!
 
Chakula ni mchana tu mboga nyingi na kupunguza ugali na ubwabwa, asubuhi green tea na limao au kausha, jioni kula ni vegetable soups, supu no chapati na wanga wa namna yoyote ile na kula mwisho saa 1 jioni.
Mazoezi ni kutembea na siyo kukimbia mwendo wa kasi wastani wa 10km au zaidi kila siku hakuna weekend wala excuse yoyote, mambo ya gym na vyuma achana nayo yanakatisha tamaa na kujiumiza..
Hii vita ni kali sana mimi mwenyewe nipo napambana..
 
Ila maisha haya jamani! Usukumani asubuhi ugali wa mchungaji, mchana ugali na usiku ugali. Wamebadili sana wali nao lazima usindikizwe na ka ugali. Lakini huoni wakinenepeana! Utasema kazi wanazozifanya mbona na Sisi huku mjini tunapiga kazi hizo hizo lakini hatukondi?
 
Sijui kwanini imekuwa hivyo

Mimi nikienda Kijiji huko Kanda ya Ziwa, unatengewa wali kama starter, baada ya dakika 10 unaletwa ugali mkubwa (mwekundu) na samaki

Ukiwacheki wenyeji, hata dalili ya unene hawana 🙌

Sasa huku town ukila hivyo, saa ngapi usipate mwili kama wa marehemu Captain Komba
 
Kuna Ring linauzwa 15k na bench linauzwa 250k hadi 200k,ukiwa serious miezi mitatu kitambi kinaisha
15K ndio shilingi ngapi?


Na ni LB ngapi kwa bei hiyo?


Bench niko nalo nililiproduce mimi mwenyewe na ikitokea mtu anataka kunipatia tender juu ya hilo karibu.
 
Mtaka mawili ,moja humponyoka.
 
Kumantain lazima uwe na hela ya mbogamboga Maana Familia hawataki hiyo michemsho ya mboga mboga so budget nyingine iwepo.
Yaani Wewe ni mwendo wa harage, dagaa nyama, mbogamboga, tunda na maji kwa wingi chai unaachana nayo.

Maandazi, chapati, vitumbua na vitafunwa vya wanga na mafuta tupakule
 
Tunakula sana ma vyakula ya wanga kupitiliza, mwaka mzima ni ugali wali, tutaachaje kupata vitambi

Inahitaji discipline ya Hali ya juu ya mazoezi na uchaguzi sahihi wa diet, la sivyo ni kitambi pro max
Mmmh mbona wachina, wajapan, wathailand, indonesia n.k huko watakula sana wali lakini hawana vitambi na wana life span ndefu kuliko sisi wabongo??fafanua mkuu.
 
Muongo wewe, ulaya watu hawali hovyo hovyo tena hawajui hayo maugali na wapo makini sana na lishe bora, umelishwa maneno ya vijiweni na wewe ukaingia kingi. Ulishawai kuona rais au hata mawaziri wa nchi za Ulaya wana vitambi?? waafrika mnakula hovyo hovyo sana na tena asilimia 95 ya mavyakula ni wanga tu ndio maana hata life span yenu ni ndogo 60 tu mtu kachoka balaa na anaitwa mzee wakati nchi za ulaya huyo mtu bado kabisa anadai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…