Hujaeleweshwa vizuri na hao NSSF.
Mimi nilikuwa nafanya kazi sehemi mkataba ukaisha nikasubiri muda ulivyofika nikajaza maombi ya kulipwa pesa yangu,nikaambiwa kwakuwa ni professional unalipwa asilimia 33 ya mshahara wako wa mwisho na fedha nyingine utapata baada ya miezi 18 kama hujapata kazi
Nikakubali,nililipwa asilimia 33 kwa muda wa miezi sita kama kawaida,baada ya miezi 18 kupita nikaenda kudai kilichobaki hapo ndipo nilishangaa,waliniambia kiasi kilichobaki siwezi kupata chote,nitapata kiasi fulani kwa formula hii.
Fedha nitakayopata= fedha iliyobaki baada ya kulipwa awamu ya kwanza-(minus) fedha jumala niliyochukua kwa muda wa miezi sita.
Mfano jumla ya michango yote= 4,000,000
Ukalipwa milioni 1,400,000 kwa muda wa miezi sita,itabaki 2,600,000.
Hivyo baada ya miezi 18 utalipwa.
2,600,000-1,400,000 (uliyochukua)= 1,200,000
Fedha utakayoipata ni 1,200,000/=