Nawezaje kupata vibali toka SIDO, TFDA na TRA?

Complicator

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
2,198
Reaction score
3,580
Poleni na shughuli za utafutaji wajasiriamali.

Mimi ni kijana mjasiriamali,kwa sasa natengeneza sabuni za maji na pia Niko mbioni kutengeneza za vipande na kisha mafuta ya ngozi na nywele.

Ninapenda sana uzalishaji wa bidhaa na biashara yake,lakini tangu nimeanza kuna changamoto kadhaa ninazipata kiasi cha kuja hapa kuomba ushauri.

1.Upatikanaji wa Malighafi na Gharama zake.

Hii ni moja kati ya changamoto za msingi sana
Kwa hapa Mbeya tunategemea maduka mawili au matatu tu kwa ajili ya kununua malighafi za kutengeneza bidhaa tajwa.

Hali hii ya uchache wa maduka haya imepelekea malighafi hizi kuuzwa bei juu sana na bei zake kutokua na consistency, kila siku zinaongezwa bei bila utaratibu.

Hii inafanya nifikiri pia kuswitch kutoka biashara yangu na kufanya hii ya malighafi,lakini kama kuna mtu anafikiri anaweza ungana na Mimi kufanya hii tuwasiliane tuunganishe nguvu.

Pia naomba kwa mwenye kujua chimbo la bidhaa hizi ni lipi kwa huko DSM...Ili siku moja niwe nazifata mwenyewe,hii itasaidia sana kupunguza gharama za uzalishaji.

3. Uhakika na Muendelezo kwenye masoko.

Changamoto nyingine ni hii,kiuhalisia bidhaa hizi zina wateja lakini shida ni namna ya kua na soko la uhakika kiasi cha kuweza kuingiza fedha Mara kwa Mara,kwa sasa unaweza kuuza Lita 20 kila baada ya wiki mbili au tatu,hii si nzuri kibiashara.

Hapa pia naomba kwa mwenye kuweza kuniunga mkono anunue bidhaa zangu kwani nazitengeneza kwa uaminifu mkubwa tofauti kabisa na bidhaa zingine sokoni.

3. Kupata uhalali wa kuuza bidhaa hizi.

Hapa nazungumzia kupata vibali toka SIDO,TFDA NA TRA na kisha kuwa huru na halali kufanya biashara hii ambayo inahusisha afya za watu.

Kwa mwenye kujua utaratibu wa kupata vibali hivi anisaidie.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa hatua hiyo kubwa sana, kuhusu vibali anzia kwenye ofisi za sido, wale watakusaidia kupata Tbs, na Tfda wao ni kama mawakala wao huku mikoani. Baada ya hapo utaenda Tra kwa ajili ya kufungua file na kupewa tin
 
kiuhalisia, bidhaa ulizozitaja zinaweza zikawa na madhara, kiafya, kiuchumi na kimazingira hivyo kabla ya uzalishaji wake kibiashara unatakiwa kudhibitisha ubora wake kwa SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS), na hii ni baada ya kutoka SIDO
 
Hongera kwa kuwa mjasiriamali
Fuata hatua hizi
1. Kajisajiri TIN TRA
Ukipata TIN
2. Hatua inayofuata ni kuandika barua ya utambulisho wa biashara yako kwenda SIDO. SIDO watakuja kukutembelea kuhakiki biashara yako na kukupa ushauri wa kitaalam nk. Kama umefuzu utakuwa kila unapotaka kupata sehemu yyt kibali mathalani manispaa kwa ajili ya leseni (kuzalisha na kuuza), ubora TBS, Usalama wa bidhaa TFDA nk utakuwa unawaandikia barua SIDO, then wao wanaandika barua kwenda taasisi husika kwa kukutambulisha kama mwanachama wao na hivyo kusaidiwa kwa mujibu wa taratibu za taasisi husika. Mwongozo huo hapo picha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana,nimeshapata namba ya meneja wa mkoa na kesho ninakutana naye uso kwa uso.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la sabuni nyingi za tanzania viwango vya ubora ni zero kabisa
 
Ukiweza kutengeneza sabuni ya maji kwa ajili ya kuoshea magari na vyombo utafanya biashara zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…